Yametimia: Unai Emery Atupiwa Virago Arsenal Baada Ya Miezi 18

29th November 2019

LONDON, Uingereza- Klabu ya Arsenal wameamua kuvunja mkataba wao na kocha Unai Emery ikiwa ni siku moja tu tangu timu hiyo ilipopoteza mchezo wa Europa kwa kufungwa 2-1 na Frankfurt ya Ujerumani kwenye dimba la Emirates.

Unai Emery
Unai Emery
SUMMARY

"Kwa sasa timu itakuwa chini ya aliyekuwa kocha msaidizi Freddie Jungberg ambaye tunaamini ataweza kuisukuma timu kwenda mbele kwa kipindi hiki kifupi," imesomeka taarifa ya Arsenal.

Kipigo dhidi ya Frankfurt kimefikisha idadi ya mechi saba kwa Washika Bunduki hao bila kupata ushindi kwenye michuano yote. Huo ni mfululizo mbaya sana wa matokeo ukikaribia kuvunja rekodi ya kocha George Graham ambaye yeye alifikisha mechi 8 mfululizo bila ushindi mwaka 1992.

Mara ya mwisho Arsenal kuibuka na uhindi ilikuwa ni kwenye mechi nyingine ya Europa ambapo waliwafunga Vitoria kwa mabao 3-2.

Arsenal ambao wanashika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 18 baada ya kushuka dimbani mara 13. Hata hivyo kikosi hicho hakijaibuka na ushindi kwenye EPL tangu mara ya mwisho walipowafunga Bournemouth bao 1-0, Oktoba 6.

"Maamuzi haya yamefikiwa ni kutokana na kiwango kibovu cha timu na matokeo ambayo hayaridhishi kwasasa kwenye michuano mbalimbali"

"Kwa sasa timu itakuwa chini ya aliyekuwa kocha msaidizi Freddie Jungberg ambaye tunaamini ataweza kuisukuma timu kwenda mbele kwa kipindi hiki kifupi," imesomeka taarifa ya Arsenal.

Unai Emery Ni Nani?

Kocha Unai Emery alijiunga na Arsenal mwanzo wa msimu wa 2018-19 ambapo kwa mara ya mwisho alifanya kazi ndani ya kikosi cha PSG kwa misimu miwili na kufanikiwa kunyakuwa taji la Ligue 1.

Kabla ya kujiunga na PSG kocha huyo aliwahi kuzifundisha timu kadhaa za Hispania zikiwemo Valencia na Sevilla ambayo aliiongoza kubeba taji la Europa mara tatu mfululizo katika kipindi chake.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya