Ligi Kuu Bara: Azam Kuendeleza Moto Leo Dhidi Ya Wapiga Kwata JKT Tanzania?

1st December 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Leo ligi kuu bara inaendelea tena kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye dimba la Azam Complex ambapo wenyeji Azam FC watawaalika wapiga kwata wa JKT Tanzania.

Azam FC
Azam FC
SUMMARY

Kwenye msimamo Azam wapo nafasi ya nne wakiwa na alama 19 baada ya kushuka uwanjani mara 9 huku JKT Tanzania wakiwa nafasi ya 3 wakiwa na alama 15 baada ya kushuka dimbani mara 11.

Azam wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi mnono wa mabao 5-0 walioupata kwenye mchezo wao mwisho walipocheza dhidi ya Alliance ya Mwanza siku ya Jumanne.

Wakati Azam wakiwa na kumbukumbu hiyo JKT Tanzania wao nao wana kumbukumbu ya kuwafunga 2-1 wanajeshi wenzao Ruvu Shooting kwenye mchezo wao wa mwisho uliofanyika siku tatu zilizopita.

JKT Tanzania wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa dhahiri wanakumbuka jinsi walivyo nyanyaswa na Azam kwa kupigwa mabao 6-1 kwenye mchezo wa ligi waliokutana msimu uliopita ndani ya dimba la Azam Complex sehemu ambapo leo mchezo utafanyika.

Kiujumla ni kwamba tangu walipopanda daraja msimu uliopita JKT Tanzania hawajawahi kuwafunga Azam zaidi walipokea vichapo kwenye mechi zote mbili za nyumbani na ugenini.

Kwenye msimamo Azam wapo nafasi ya nne wakiwa na alama 19 baada ya kushuka uwanjani mara 9 huku JKT Tanzania wakiwa nafasi ya 3 wakiwa na alama 15 baada ya kushuka dimbani mara 11.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya