Mida Ya Kubeti: Arsenal Ndani Ya Maisha Mapya Kukabiliana Na Norwich Ugenini Leo
1st December 2019
NORWICH, Uingereza- Siku mbili baada ya kumtupia virago kocha wao Unai Emery, Arsenal leo wanashuka kwenye dimba la ugenini kuchezo dhidi ya Norwich City kwenye mchezo wa 14 wa ligi kuu ya Uingereza.
Upo tayari kushinda MAMILIONI leo?
Bet mechi kali za leo kupitia SportPesa bila kutumia bando lako ujishindie MAMILIONI kwa JERO au zaidi.
Bofya HAPA kubet sasa
Arsenal leo wanaingia dimbani wakiwa chini ya kocha wa mpito ambaye ni mchezaji wao wa zamani Freddie Lujngberg na watakuwa wanasaka ushindi wa kwanza kwenye ligi ambao waliokosa tangu mara ya mwisho walipowafunga Bournemouth Oktoba 6.
Norwich wamekutana na Arsenal mara 16 kwenye historia ya ligi kuu ambapo katika mechi hizo wao wameshinda mara 2 tu huku Arsenal wakishinda mara 8. Mechi 6 zimeisha kwa sare.
Mechi zao tano za mwisho kukutana Arsenal wameshinda mara 4 huku mechi moja ikiisha kwa sare.
Arsenal hawajashinda hata mechi moja kati ya tano zilizopita kwenye ligi msimu huu huku Norwich wao wakishinda mechi yao iliyopita dhidi ya Everton lakini wakifungwa mara tatu na kutoka droo mechi moja kwenye mechi zao tano za mwisho.
Man United v Aston Villa
Kibarua kingine leo ni ndani ya dimba la Old Trafford ambapo Man United chini ya kocha wao Ole Gunnar Solskjaer watakuwa nyumbani wakiwaalika Aston Villa.
Man United watakuwa na nafasi ya kuwarejesha kwenye kikosi chao cha kwanza wachezaji wao nyota ambao walipumzishwa kwenye mechi iliyopita ya mchezo wa Europa dhidi ya Astana ugenini.
Mechi baina ya timu hizo kwa siku ya leo itakuwa ni ya 49. Kwenye mechi 48 zilizopita Man United wamewafunga Villa mara 34 huku Villa wao wakishinda mara 3 tu. Mechi 11 zimekwisha kwa sare.
Katika mechi zao tano za mwisho kukutana kabla ya mchezo wa leo, Man United wameshinda mechi 4 na mchezo mmoja umekwisha kwa sare.
Fomu ya timu hizo mbili kwasasa haitofautiani sana. Man United wameshinda mechi mbili, wamesuluhu mechi mbili na wamefungwa mchezo mmoja kati ya michezo yao mitano iliyopita kwenye ligi.
Villa wao pia wameshinda michezo miwili na wamefungwa kwenye michezo mitatu kukalimisha idadi ya michezo yao mitano.
Leicester City V Everton
Kocha Marco Silva wa Everton huenda akaoneshwa mlango wa kutokea endapo atakubali tena kichapo kwenye mechi hii dhidi ya Leicester City.
Kwa bahati mbaya sana leo wanakutana na Leicester City ambayo ni ya moto kweli kweli na uwezekano wa kufungwa mabao mengi upo hasa ukizingati fomu ya vikosi vya timu zote mbili kwasasa.
Leicester City ndiyo wanaoshika nafasi ya pili kwenye ligi wakiwakimbiza Liverpool na wakishinda mechi ya leo maana yake watakuwa wamepunguza gepu la pointi kutoka 11 hadi kufikia 8.
Timu hizo leo zinakutana kwenye mchezo wa 27 ambapo kwenye mechi zao 26 zilizopita Leicester City wana ushindi mara 5 huku Everton wakiwa wameshinda mara 8. Mechi 13 zimekwisha kwa sare baina yao.
Mechi zao tano walizokutana hivi karibuni hakuna sare. Everton wameshinda mara tatu na Leicester wameshinda mara 2. Mechi ya mwisho kukutana kwenye uwanja wa King Power, Everton waliibuka na ushindi wa 2-1 ugenini.
Leicester City wameshinda mechi zao zote tano zilizopita za ligi msimu huu wakati Everton wameshinda mechi 2 wamefungwa 2 na wametoka sare mchezo mmoja.
Mechi Nyingine
Wolves v Shefield United
Imeandaliwa na Badrudin Yahaya