Tetesi: Formula 1 Wakataa Uwezekano Wa "Super Sunday"

9th November 2019

LONDON, Uingereza- Mamlaka zinazosimamia mchezo wa mashindano ya magari maarufu kama Formula 1 zimekanusha uwezekano wa kufanyika kwa kitu kilichopachikwa jina la "Super Sunday".

Formula 1
Formula 1
SUMMARY

Tetesi za uwezekano wa kubadilishwa kwa ratiba hiyo zilizidi kushika kasi na ndipo wenye mamlaka wamekuja na kukanusha kwa kusema kuwa hakutakuwa na hiyo "Super Sunday" badala yake mfumo ule ule wa siku tatu utaendelea kutumika.

Najua hapo haujaelewa, sasa twende sawa! Ni kwamba wakati wa msimu wa Formula 1 unaendelea, ilipofika Japan GP kulikuwa na shida kwani wiki ambayo kulipangwa mbio kufanyika ilibainika hali ya hatari ya kimbunga.

Kutokana na suala hilo baadhi ya shughuli zilisimamishwa ikiwemo mazoezi ya mchujo "practice" ambapo kikawaida huwa zinaanza Ijumaa hadi Jumamosi na siku ya Jumapili ndiyo mashindano hufanyika.

Hata hivyo nchini Japan kutokana na suala hilo, mamlaka za Formula 1 zilisimimisha shughuli za Ijumaa na Jumamosi na badala yake shughuli zote zikahamishiwa Jumapili ambao watu walimaliza kila kitu.

Baada ya tukio hilo madereva na mashabiki wengi walifurahishwa na ratiba ile na wengi wao waliomba msimu ujao ikibidi ratiba iwe ni ya siku moja tu ambayo ni Jumapili badala ya siku tatu kama ilivyozoeleka.

Tetesi za uwezekano wa kubadilishwa kwa ratiba hiyo zilizidi kushika kasi na ndipo wenye mamlaka wamekuja na kukanusha kwa kusema kuwa hakutakuwa na hiyo "Super Sunday" badala yake mfumo ule ule wa siku tatu utaendelea kutumika.

"Niwe muwazi tu kwamba kulingana na kanuni zetu pamoja na watu wengine tunaoshirikiana nao hatutaweza kubadili ratiba ya siku tatu na badala yake tutaendelea kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali," amesema Ross Brawn.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya