Tennis: Stefanos Tsitsipas Uso Kwa Uso Na Dominic Thiem Fainali Ya ATP Leo
17th November 2019
LONDON, Uingereza- Hayawi Hayawi, Sasa Yamekuwa! Sasa ni rasmi natangaza kuwa fainali ya michuano ya ATP (Nane Bora) msimu huu itakuwa ni kati ya wachezaji tenesi vijana hodari Stefanos Tsitsipas ambaye atacheza dhidi ya Dominic Thiem.
Mchezo huo wa fainali utakaochezwa leo utakuwa ni mgumu na wakukamiana sana hasa kwa vijana hao ambao wamekuwa na michuano bora sana msimu huu.
Hii ni mara baada ya vijana hao kufanya kazi ya ziada na kuangusha mibuyu kwenye michezo yao ya nusu fainali iliyofanyika usiku wa kuamkia leo.
Kwa upande wake Tsitsipas mwenye umri wa miaka 21 yeye amefanikiwa kumtoa mashindanoni Rodger Federer, 38 kwa kumfunga jumla ya seti 6-3 6-4.
Naye Thiem, 26 amemuangusha bingwa mtetezi wa michuano hiyo Alexander Zverev kwa jumla aya seti 7-5 6-3.
Mchezo huo wa fainali utakaochezwa leo utakuwa ni mgumu na wakukamiana sana hasa kwa vijana hao ambao wamekuwa na michuano bora sana msimu huu.
Tofauti na Thiem, Tsitsipas yeye ndiyo ameshiriki michuano hii kwa mara ya kwanza kabisa kwenye maisha yake lakini suala la kuvutia zaidi ni kwamba wote hawajawahi kushinda taji la namna hiyo.
Michuano ya ATP ni michuano ya funga mwaka unaweza kusema ambayo huwa inachezwa mwisho wa msimu wa tenesi. Wanaoshiriki ni wachezaji wanaoshika nafasi nane za juu kwa ubora duniani.
Mashindano huanza kwa wachezaji hao kugawanywa kwenye makundi mawili ambapo kila kitu litatoa washindi wawili wa juu ambao wanaingia nusu fainali.
Kwenye michuano ya mwaka huu walioshiriki kwa ujumla ni Rafael Nadal, Novak Djokovic, Rodger Federer, Dominic Thiem, Stefanos Tsitsipas, Matteo Berrettin, Alexander Zverev na Daniil Medvedv.
Imeandaliwa na Badrudin Yahaya