Tanzania Yafuzu Kombe La Dunia 2022 Kwa Wenye Ulemavu

12th October 2019

BENGUELA, Angola -Timu ya taifa ya soka ya watu wenye ulemavu imefanikiwa kufuzu michuano ya kombe la duniani itakayofanyika mwaka 2022.

Timu ya Taifa
Timu ya Taifa
SUMMARY

Ikumbukwe kwamba hii ilikua ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa kama haya ikiwa inatimiza pia mwaka mmoja pekee tangu kuundwa kwa shirikisho linalosimamia mchezo huo hapa nchini.

Licha ya kupoteza mchezo wa kutafuta nafasi ya mshindi wa tatu ikifungwa magoli 2-1 na Liberia katika mashindano ya Afrika, bado Timu ya taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu kwa wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’, imefanikiwa kufuzu kuliwakilisha bara la Afrika katika michuano hiyo itakalofanyika kati ya Uingereza au Costa Rica.

Tembo Warriors imefanikiwa kupata nafasi hiyo ikiwa ni kati ya timu 4, nyingine zikiwa ni Liberia (washindi wa tatu), Nigeria (washindi wa pili) na Angola ambao wamekuwa mabingwa  wa Afrika wa mashindano hayo.

Chanzo TFF