Riadha: Eliud Kipchoge Aweka Rekodi Ya Dunia Kwenye Mbio Za Marathon Vienna

12th October 2019

VIENNA, Australia- Mwanariadha raia wa Kenya, Eliud Kipchoge ameweka rekodi ya dunia kwenye mbio za marathon baada ya kufanikiwa kukimbia kwa muda wa saa 1:59:40.

Eliud Kipchoge
Eliud Kipchoge
SUMMARY

Ikumbukwe kuwa Mwaka 2017, Kipchoge alidhaminiwa na Nike huko Monza nchini Italia kwa ajili ya tukio kama hili alilofanya jana lakini alishindwa kutimiza ndoto hizo baada ya kuzidisha sekunde 26.

Hiyo inakuwa ni rekodi kwenye mbio hizo tangu mashindano hayo yalipoanzishwa kwani hakuna mwanadamu ambaye amewahi kukimbia kwa muda wa chini ya saa mbili kwenye mbio hizo za Kilometa 42.

Hata hivyo rekodi hiyo haitatambuliwa rasmi kwenye takwimu za dunia kwakuwa Kipchoge alikuwa ni mwanaridhaa pekee aliyeshiriki mbio hizo akiungana na pacemakers wapatao 41 wakiwemo wanariadha wa zamani na washindi wa michuano ya olimpiki.

Kipchoge, 34, ni bingwa mtetezi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki na pia hadi sasa anashikilia rekodi ya dunia ya kukimbia kwa muda wa saa 2:01:39 aliyoiweka kwenye mashindano ya Berlin, Septemba, mwaka jana.

Mwanariadha huyo mkongwe amekuwa akijaribu kuvunja rekodi hiyo mara kwa mara bila mafanikio lakini amekuwa akirudia tena na tena bila kuchoka.

Ikumbukwe kuwa Mwaka 2017, Kipchoge alidhaminiwa na Nike huko Monza nchini Italia kwa ajili ya tukio kama hili alilofanya jana lakini alishindwa kutimiza ndoto hizo baada ya kuzidisha sekunde 26.

Kama hiyo haitoshi mwaka huu tena kampuni ya Ineos iliyochini ya, Bilionea wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe wamemdhamini tena kwa ajili ya shughuli hiyo na kumuwezesha Kipchoge ambapo safari hii sasa ametimiza ndoto zake.

"Nimekuwa nikijaribu mara kwa mara kufanikisha jambo hili na ushindi huu wa leo unaonesha kuwa uwezo wa mwanadamu hauna mipaka," amesema Kipchoge akiwa na uso wenye furaha.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya