Pyramids vs Yanga: Ni Mechi Ya Kufa Au kupona Kwa Timu Zote Mbili

3rd November 2019

CAIRO, Misri- Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga, wako nchini Misri ambapo usiku wa leo Jumapili Novemba 03 2019, watashuka katika uwanja wa 30th June kuikabili Pyramids FC.

Yanga SC
Yanga SC
SUMMARY

Zahera amesema amewapanga vyema walinzi wake wanne wa nyuma na kuwataka kuwa makini na washambuliaji wa Pyramids hasa Erick Traore na Mohamed Said ambao waliwasumbua na kuwafunga mabao hayo mawili.

Mchezo huo ni wa pili baina ya timu hizo baada ya Pyramids FC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Mwanza wiki iliyopita.

Katika mchezo wa leo ambao umepangwa kuanza majira ya saa 3:00 usiku Yanga wanahitaji ushindi wa kuanzia mabao mawili ili kufuzu hatua ya makundi.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera, amesema wamejipanga kikamilifu na anamatumaini ya kupata ushindi katika mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

Katika mchezo wa leo Zahera atakosa huduma ya beki mzoefu Kelvin Yondani aliyeonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kwanza lakini anafurahi kurejea kwa Mghana, Lamine Moro ambaye amemaliza kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata dhidi ya Zesco United.

Kocha huyo amesema leo kikosi chake kitakuwa na mabadiliko kidogo tofauti na kile kilichoanza mchezo uliopita ambapo amepanga kuanzisha washambuliaji wawili.

Zahera amesema amewapanga vyema walinzi wake wanne wa nyuma na kuwataka kuwa makini na washambuliaji wa Pyramids hasa Erick Traore na Mohamed Said ambao waliwasumbua na kuwafunga mabao hayo mawili.

Jana usiku kikosi cha Yanga kilifanya mazoezi katika uwanja wa 30th June ambao mchezo huo utapigwa.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed