Ndondi: Tyson Furry Ageukia Kwenye Mieleka, Sasa Kuzichapa Na Braun Strowman

13th October 2019

RIADH, Saudi Arabia- Bingwa wa zamani wa masumbwi ya uzito wa juu duniani Tyson Furry anatarajia kupanda ulingoni Oktoba 31, mwaka huu kuzichapa dhidi ya Braun Strowman kwenye ulingo wa mieleka

Braun Strowman
Braun Strowman
SUMMARY

"Unarukia kwenye dunia yangu lakini nikwambie tu mikono yangu hii itakuangusha chini na dunia nzima itajua kuwa kitu gani mimi nimefanya," amesema Strowman.

Furry, 31, ameonekana mara mbili kwenye michezo ya mieleka kwa wiki za hivi karibuni na sasa ameshaanza bifu na Strowman.

Wakati akizungumza kuhusu mpambano huo, Furry amesema kuwa hamuogopi mtu na yupo tayari kumuangusha Strowman.

Naye Strowman amemuonya Furry kwakumwambia kuwa kwenye mieleka watu hawavai gloves.

"Unarukia kwenye dunia yangu lakini nikwambie tu mikono yangu hii itakuangusha chini na dunia nzima itajua kuwa kitu gani mimi nimefanya," amesema Strowman.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya