Ndondi: Hassan Mwakinyo Apania Kumpiga Mfilipino Kwa KO

1st November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Bondia namba moja uzito wa kati Afrika Hassani Mwakinyo, amesema maandalizi yake kueleke pambano la Novemba 29 dhidi ya Mphilipino, Arnel Tinampay yanakwenda vizuri na unauhakika wa ushindi wa KO.

Hassan Mwakinyo
Hassan Mwakinyo
SUMMARY

Tinampay anatarajiwa kuwasili nchini siku 13 kabla ya pambano hilo na atatembelea sehemu mbalimbali ikiwemo kambi anayofanyia mazoezi Mwakinyo kule Tanga na baadaye atarudi Dar es Salaam kuendelea na maandalizi kwenye Gym ya Mlimani City na Mbagala.

Pambano hilo limepangwa kufanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ambapo Mwakinyo anayedhaminiwa na kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa amedhamiria kumsambaratisha mapema mpinzani wake.

Akizungumza na Mtandao wa SportPesa News, Mwakinyo amesema anatamani tarehe 29 ifike ili aweze kuwadhihirishia Watanzania kile anachokisema.

"Sina mpango wa kwenda nje kupiga kambi ya kujiandaa na pambano hili nitabaki nyumbani Makorora Tanga hadi tarehe zitakaribia na nimepania kumchakaza mapema kabla ya raundi ya 10, kwani ngumi zangu zinauma sana," amesema Mwakinyo.

Ushindi wa KO

Kwa upande wake Promota wa pambano hilo James Msangi amesema maandalizi ya pambano hilo yanakwenda vizuri na wanauhakika bondia wao Mwakinyo atashinda kwa KO pambano hilo.

Amesema ili kuhakikisha burudani hiyo inawafikia Watanzania wote wameingia mkataba na kituo cha Azam Media ili kurusha mubashara pambano hilo.

Tinampay Kuja Mapema

Msangi amesema mpinzani wa Mwakinyo, Tinampay anatarajiwa kuwasili nchini siku 13 kabla ya pambano hilo na atatembelea sehemu mbalimbali ikiwemo kambi anayofanyia mazoezi Mwakinyo kule Tanga na baadaye atarudi Dar es Salaam kuendelea na maandalizi kwenye Gym ya Mlimani City na Mbagala.

Mabondia hao wanakutana kila mmoja akiwa kinara kwenye taifa lake Mwakinyo ni namba moja Tanzania na Afrika na Tinampay yeye ni namba mbili nchini kwao Phillipins na anarekodi ya kushinda  kwa KO.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed