NBA: San Antonio Spurs Wakwaa Kisiki Mbele Ya Dallas Mavericks
19th November 2019
DALLAS, Marekani- Luka Doncic amefunga vikapu 42 ambapo ni idadi kubwa zaidi kwenye maisha yake ya mpira wa kikapu kwenye mechi moja na kuiwezesha timu yake ya Dallas Maverick kuibuka na ushindi wa 117-110 dhidi ya San Antonio Spurs.
Kwa upande wa Spurs, DeMar DeRozan ndiye aliyekuwa shujaa kwa kufunga alama nyingi zaidi 36 ambazo ni nyingi kwake msimu huu ndani ya mechi moja.
Mbali na alama hizo 42 lakini pia Doncic aliweza kufanta rebound 11 na assisti 12 kwenye mchezo huo ambao ni wa pili mfululizo kwa timu hiyo.
Wachezaji wengine wa Dallas waliochangia ushindi huo ni Finney- Smith ambaye amefunga alama 22 huku Kristapas Porzingis akiongeza 18. Jalen Brunson alifunga vikapu 11.
Kwa upande wa Spurs, DeMar DeRozan ndiye aliyekuwa shujaa kwa kufunga alama nyingi zaidi 36 ambazo ni nyingi kwake msimu huu ndani ya mechi moja.
James Harden v Russell Westbrook
Manguli wawili wa Houston Rockets, James Harden na Russell Westbrook kwa pamoja wamefunga vikapu 64 na kuiwezesha timu yao kushinda kwa jumla ya alama 132-108 dhidi yawageni wao Portlaind Trail Blazzers.
Harden kwa upande wake yeye alifunga alama 36 wakati Westbrook akifunga 28 na kuongeza rebound 13 na assist 10 kwenye mchezo huo.
Huo ni ushindi wa 8 mfululizo kwa Rockets ambao kwa mechi za hivi karibuni wamebebwa sana na moto wa Harden.
Matokeo Mengine:
San Antonio Spurs 110-117 Dallas Mavericks
Portland Trail Blazers 108-132 Houston Rockets
Boston Celtics 95-85 Phoenix Suns
Oklahoma City Thunder 88-90 LA Clippers
Milwaukee Bucks 115-101 Chicago Bulls
Minnesota Timberwolves 112-102 Utah Jazz
Indiana Pacers 115-86 Brooklyn Nets
Charlotte Hornets 96-132 Toronto Raptors
Cleveland Cavaliers 105-123 New York Knicks
Imeandaliwa na Badrudin Yahaya