NBA: Moto Wa Kawhi Na Paul George Umewazidi Kimo Timu Pinzani
27th November 2019
LOS ANGELES, Marekani- Bala zitooo! Hivi ndivyo unavyoweza kusema ukiwaongolea nyota wawili wa LA Clippers, Kawhi Leonard na Pau George ambao kwasasa wametengeneza "Combo" hatari inayogawa dozi za maana kwenye ligi ya mpira wa kikapu Marekani.
Nyota hao wote ni wapya kwenye timu hiyo. Walisajiliwa mwanzo wa msimu huu. Hata hivyo Kawhi yeye alianza kucheza tangu mwanzo lakini George alichelewa kuanza kukitumikia kikosi chake kutokana na majeruhi.
Kwa mara nyingine tena alfajiri ya leo wachezaji hao wameungana kuwaangamiza Dallas Mavericks kwa jumla ya vikapu 114-99 na kufanya timu yao kuibuka na ushindi wa sita mfululizo.
Kwasasa hakuna timu inayoogopesha kukutana nayo kwenye NBA kama Clippers ambao hawabip wao wanapiga tu.
Moto Huo Umtokea Wapi?
Nyota hao wote ni wapya kwenye timu hiyo. Walisajiliwa mwanzo wa msimu huu. Hata hivyo Kawhi yeye alianza kucheza tangu mwanzo lakini George alichelewa kuanza kukitumikia kikosi chake kutokana na majeruhi.
Wakati George anapona, Kawhi naye alikuwa ameumia na alikaa nje kwa mechi nne. Tangu Kawhi aliporudi dimbani na kukutana na George balaa ndiyo lilianzia hapo.
Ule ubora ambao walianza nao tangu mwanzo wa msimu kutokana na uwezo wa Kahwi umeongezekana mara mbili baada ya kuungana na George na sasa wawili hao wamecheza mechi sita mfululizo pamoja huku mechi zote wakishinda kwa kishindo.
Mechi Dhidi Ya Dallas
Kwenye mechi ya alfajiri ya leo, Kawhi amefunga alama 28 na George ameongeza zake 26 huku 17 akizifunga ndani ya robo ya kwanza. Wachezaji hao wawili kwasasa wanafurahia maisha mazuri ya kucheza pamoja kama ilivyo kwa mashabiki wa Clippers duniani kote.
Luka Doncic kama kawaida yake aliongoza ufungaji kwa upande wa Dallas akifunga alama 22 na kufanya rebound 8 huku Kristaps Porzingis akifunga 15 kwa upande wa timu yao.
Lou Williams akitokea benchi naye kama kawaida ameendeleza moto wake mzuri wa kufunga alama kwenye kila mchezo akipata pointi 21 ikiwa ni mfungaji bora wa tatu kwa upande wa Clippers nyuma ya Kahwi na Geoge kwenye mchezo huo.
Matokeo Mengine
Los Angeles Clippers 114-99 Dallas Mavericks
Washington Wizards 104-117 Denver Nuggets
Imeandaliwa na Badrudin Yahaya