NBA: LeBron James Aupiga Mwingi, LA Lakers Wakishinda Mechi Ya Sita Mfululizo

6th November 2019

LOS ANGELES, Marekani- LeBron James amefunga alama 30 akifanya rebound 10 na assisti 11 wakati akiisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa 118-112 dhidi ya Chicago Bulls.

Lebron James
Lebron James
SUMMARY

Lakers ambao muda mwingi wa mchezo walikuwa nyuma ya Bulls walifanikiwa kupindua matokeo kwenye robo ya nne ambapo waliibuka na ushindi wa vikapu 38-19.

Ushindi huo ni wa sita mfululizo kwa LA Lakers ambao wamewasha moto mkubwa tangu walipokubali kipigo kutoka kwa majirani zao LA Clippers kwenye mchezo wa kwanza tu wa msimu.

Quinn Cook kwenye mchezo huo naye alifunga vikapu 17 akitokea benchi wakati mshambuliaji wakutegemewa wa timu hiyo, Anthony Davis yeye alifunga vikapu 15 na rebound saba wakati aliporudi kwenye mji wa Chicago mahala ambapo amezaliwa.

Lakers ambao muda mwingi wa mchezo walikuwa nyuma ya Bulls walifanikiwa kupindua matokeo kwenye robo ya nne ambapo waliibuka na ushindi wa vikapu 38-19.

Matokeo hayo ya kwenye robo ya nne ndiyo kwa kiasi kikubwa yamechagiza ushindi wa jumla kwenye mchezo huo.

Zach LaVine amefunga vikapu 22 kwa upande wa Bulls huku Otto Porter Jr na Coby White wao wakifunga alama 18 kila mmoja.

Matokeo Kamili: 

Los Angeles Lakers 118-112 Chicago Bulls

Miami Heat 89-109 Denver Nuggets

San Antonio Spurs 100-108 Atlanta Hawks

Boston Celtics 119-113 Cleveland Cavaliers

Orlando Magic 94-102 Oklahoma City Thunder

Indiana Pacers 120-122 Charlotte Hornets (OT)

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya