NBA: Giannis Awawashia Moto Clippers, GSW Wapokea Kipigo Cha Sita Msimu Huu

8th November 2019

LOS ANGELES, Marekani- Giannis Antetokounmpo amefunga vikapu 38, rebound 16 na kuiwezesha timu yake Milwaukee Bucks kuibuka na ushindi wa nne mfululizo baada ya kuwafunga LA Clippers kwa vikapu 129-125.

Giannis Antetokounmpo
Giannis Antetokounmpo
SUMMARY

Clippers walikuwa bila ya nyota wao Kawhi Leornad ambaye alipumzishwa ili kujiweka tayari kwa mchezo unaofuata dhidi ya Portland.

Kiwango cha Giannis msimu huu kimemfanya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya NBA kufikisha alama 200, rebound 100 na assisti 50 kwenye mechi nane za awali.

Kama umesahau basi nikukumbushe kuwa Giannis mwenye uraia wa Uturuki ndiyo MVP wa msimu uliopita na hiki anachokionesha sasa ni mwendelezo wake tu.

Clippers walikuwa bila ya nyota wao Kawhi Leornad ambaye alipumzishwa ili kujiweka tayari kwa mchezo unaofuata dhidi ya Portland.

Hata hivyo Montrezl Harrell alisimama akiziba nafasi ya nyota huyo kwa kufunga vikapu 34 ambavyo ni vingi kuwahi kufunga ndani ya mchezo mmoja tangu alipoanza kucheza, hata hivyo alama hizo hazikuweza kuwaepusha na kipigo.

Jahazi La GSW Lazidi Kuzama

James Harden amezidi kulizamisha jahazi la Golden State Warriors baada ya kufunga alama 36 na kuiwezesha timu yake ya Houston Rockets kuibuka na ushindi wa 129-112.

Warriors kwasasa wanapita kipindi kigumu baada ya kutawala mchezo huo kwa takribani miaka mitano.

Wamefungwa kwenye mchezo wa sita kati ya nane waliyoshuka dimbani msimu huu huku wakiwa wanawakosa nyota wao muhimu uwanjani.

Ukiachana na Kevin Duran aliyehama timu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu, Klay Thompson, Stephen Curry na Dryamond Green nyota hao ni majeruhi kwasasa na wameiacha timu kwenye mazingira ya kutisha.

Matokeo Mengine

Golden State Warriors 112-129 Houston Rockets

Milwaukee Bucks 129-124 LA Clippers

Philadelphia 76ers 104-106 Utah Jazz

Orlando Magic 106-107 Dallas Mavericks

Minnesota Timberwolves 121-137 Memphis Grizzlies

Chicago Bulls 113-93 Atlanta Hawks

Sacramento Kings 120-124 Toronto Raptors

New York Knicks 102-122 Detroit Pistons

Washington Wizards 106-121 Indiana Pacers

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya