Ligi Kuu Bara: Simba v Azam Nani Kutibua Rekodi Ya Mwenzake Leo Uwanja Wa Uhuru?

23rd October 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba leo wanatarajia kukabiliana na Azam FC kwenye uwanja wa taifa.

Simba vs Azam
Simba vs Azam
SUMMARY

Shinda MAMILIONI na GARI jipyaa

Usiishie tu kusubiria matokeo ya mechi! Bet mechi hii kupitia SportPesa uweze kujishindia donge nono katika masoko kibao leo.

Bofya HAPA kubet kuanzia JERO tu uingie kwenye droo ya kushinda GARI jipyaaa.

Timu hizo zinakutana zikiwa kwenye nafasi tofauti, Simba ambao ndio wenyeji ni vinara wa ligi baada ya kujikusanyia pointi 12, katika michezo minne waliyocheza wakati Azam wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi tisa baada ya kushuka dimbani mara tatu.

Katika mchezo wa leo Simba itawakosa nyota wake watatu kutokana na Majeruhi nyota hao ni Jonas Mkude, Shomari Kapombe na nahodha msaidizi Mohamed Hussein.

Pamoja na kukosekana kwa nyota hao kocha wa Simba Patrick Aussems, amesema mchezo utakuwa mzuri na wenye ushindani kwasababu zinakutana timu mbili bora Tanzania.

"Tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunzshinda lakini mchezo utakuwa mgumu kwasababu zinakwenda kukutana timu mbili bora natarajia kuona mpira ukitembea kwenye nyasi kila kona ya uwanja," amesema Aussems.

Mbelgiji huyo amesema kikosi chake kina azina kubwa ya wachezaji pamoja na kutkuwepo kwa Kapombe wako Gerson Fraga na Haruna Shamte amba wanaweza kuziba vyema mapengo yao.

Kwaupande wao Azam kupitia kwa kocha msaidizi Idd Cheche, amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili a kuwakabili Simba leo.

Cheche ambaye ataiongoza Azam baada ya kocha mpya Aristica Sioaba, kukosa vibali vya kazi amesema ni mechi ya kawaida wala haimpi presha nahiyo ni baada ya kukaa na timu muda mrefu akiiongoza mazoezini.

"Mashabiki wa Azam waje kwa wingi uwanjani kuja kushuhudia burudani Azam ikofiti na kila mchezaji amepania kuistopisha Simba kupata ushindi," amesema Cheche.

Mechi ya kulipa kisasi

Azam wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 4-2, kwenye mchezo wa mwisho waliokuta na Simba ambao ni wa Ngao ya Hisani.

Hivyo kocha Cheche ametamba kuutumia mchezo wa leo wa ligi kulipa kisasi na kufuta rekodi ya Simba yakushinda mechi zote nne mfululizo tangu kuanza msimu huu.

Vita ya Aussems na Cheche

Patrick Aussems anatambulika kwa ubora wa kutumia mbinu ambazo zimekuwa na faida ya kuipa matokeo Simba lakini leo anakwenda kukabiliana na Cheche mwenye rekodi ya kuifunga Simba ikiwa kwenye ubora kama ilivyo hii.

Cheche atakaa kwenye benchi akichukua nafasi ya Etienne Ndayiragije, kuondoshwa ni kocha mwenye mbinu nyingi hasa anapokutana na timu kubwa za Simba na Yanga na mara kadhaa huwa anashinda vita hizo 

Vita ya Richard Djodi na Meddie Kagere

Katika mchezo wa leo moja ya sehemu itakayo kuwa na mvuto ni safu za ushambuliaji za timu zote mbili ambapo Simba inawategemea Kagere na Miraji Athuman na Azam tumaini lao litakuwa kwa Djodi na Donald Ngoma

Nyota hao ndio watakao amua mpamano wa leo kwasababu wamekuwa ni makatili mbele ya uso wa lango la mpinzani huwa hawaitaji kupata nafasi nyingi kila inapotokea wanazitumia ipasavyo.

Kagere ndio kinara wa mabao kwenye ligi pamoja na timu yake ya Simba akifunga mabao sita katika mechi nne walizocheza hadi sasa Ngoma na Djodi kila mmoja amefunga bao moja moja.

Shinda MAMILIONI na GARI jipyaa

Usiishie tu kusubiria matokeo ya mechi! Bet mechi hii kupitia SportPesa uweze kujishindia donge nono katika masoko kibao leo.

Bofya HAPA kubet kuanzia JERO tu uingie kwenye droo ya kushinda GARI jipyaaa.

Imeandaliwa na Rahim Mohamed