Ligi Kuu Bara: Ruvu Shooting Kufuta Unyonge Mbele Ya Simba Leo? Fuatilia Dondoo
23rd November 2019
DAR ES SALAAM, Tanzania- Ligi Kuu Bara inandelea tena leo kwa michezo mitatu kupigwa kwenye viwanja mbalimbali hapa nchini.
Kwenye michezo 10 iliyopita baina ya timu hizo, Simba wameshinda michezo 9 huku mchezo mmoja ambao ulichezwa Oktoba 10, 2013 ulikwisha kwa sare ya 1-1.
Simba ambao ndiyo vinara wa ligi watakuwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es salaam kucheza dhidi ya Ruvu Shooting mchezo ambao unatarajiwa kufuatiliwa zaidi kwa siku ya leo.
Ruvu Shooting msimu huu wamekuja kivingine wakiwa tayari wamefanikiwa kuzifunga timu za Yanga na Azam ambazo huwa ni vigogo wa ligi.
Kwasasa wanakalia kwenye nafasi ya 9 wakiwa na alama zao 15 na leo wanakwenda kukutana na Simba ambao ni vinara wa ligi na wenye hasira baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Tanzania Prison.
Kwenye michezo 10 iliyopita baina ya timu hizo, Simba wameshinda michezo 9 huku mchezo mmoja ambao ulichezwa Oktoba 10, 2013 ulikwisha kwa sare ya 1-1.
Mbali na vipigo hivyo tisa Simba pia wamekuwa wakipa dozi nene Ruvu Shooting ikiwa kama ile ya msimu uliopita ya mabao 5-0 na ile ya msimu wa 2017-18 ambao Simba walishinda 7-0.
Fomu ya timu zote mbili kwasasa haitofautiani kwa sana. Simba wameshinda mechi 3, wamefungwa 1 na wametoka sare mechi 1 kwenye michezo yao mitano iliyopita.
Ruvu Shooting wao wameshinda mechi mbili na wamefungwa kwenye mechi 3 kati ya mechi zao 5 zilizopita.
Mbao v Azam
Mchezo mwingine mgumu kwa siku ya leo utakuwa ndani ya dimba la CCM Kirumba pale wagumu wa Mbao FC watakapowakaribisha wauza ukwaju wa Azam FC.
Tangu Mbao walipopanda daraja misimu mitatu iliyopita, Azam hawajawahi kupata ushindi kwenye mechi za CCM Kirumba. Wamefungwa mechi 1 na wametoka sare mechi mbili ikiwemo ya msimu uliopita.
Hata hivyo Azam nao wameshinda mechi zao zote walizocheza na Mbao kwenye uwanja wao wa Azam Complex.
Timu hizo zinakutana leo zikiwa na fomu inayolingana kwa asilimia 100. Azam wameshinda mechi mbili, wamefungwa mechi mbili na wametoa sare mchezo mmoja kama ilivyo kwa Mbao FC.
Mechi Nyingine Leo
Mbeya City v Singida United
Imeandaliwa na Rahee Mohamed