Ligi Kuu Bara: Namungo Yaitandika Lipuli Na Kukwea Hadi Nafasi Ya Pili Kwenye Msimamo
19th October 2019
LINDI, Tanzania -Timu ya Namungo FC, imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Lipuli FC ya Iringa.

Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa, uliifanya Namungo kujiwekea rekodi yakuwa timu ngeni kwenye ligi kwa kukaa nafasi ya pili na kuishusha Azam FC na Kagera Sugar ambayo sasa inashika nafasi ya tatu.
Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa, uliifanya Namungo kujiwekea rekodi yakuwa timu ngeni kwenye ligi kwa kukaa nafasi ya pili na kuishusha Azam FC na Kagera Sugar ambayo sasa inashika nafasi ya tatu.
Katika mechi kati ya Tanzania Prisons na Kagera Sugar timu hizo zimetoka sare yakufungana bao 1-1, mabao yote mawili yamefungwa kipindi cha pili wakianza wenyeji Tanzania Prisons kufunga bao la kuongoza dakika ya 48, kupitia kwa Ismail Azizi na Kagera Sugar wakasawazisha dakika ya 78 kupotia kwa Nossoro Kapama aliyetokea benchi.
Sare hiyo imeifanya Kagera Sugar kufikisha pointi 10, na kuishusha Azam FC iliyokuwa ikikalia nafasi hiyo baada ya kukusanya pointi tisa katika michezo mitatu iliyocheza.
Katika mchezo huo kiungo wa Kagera Sugar Zawadi Mauya, alilazimika kutolewa uwanjani dakika ya 14 baada ya kugongana na kipa wa Prisons Jeremia Kisubi na kuvuja damu puani.
Ubovu wa uwanja.
Kocha wa Kagera Sugar, amesema kiwango kibovu kilichoonyeshwa na wachezaji wake kimetokana na ubovu wa uwanja wa Sokoine ambao ulikuwa na utelezi na mabonde.
Pamoja na hivyo lakini amefurahi kuvuna pointi mmoja ambayo imemanya kupanda hadi nafasi ya tatu akilingana pointi na Namungo FC ambayo inashika nafasi ya pili baada ya ushinda dhidi ya Lipuli.
Mechi nyingine za VPL leo
Tanzania Prisons 1-1 Kagera Sugar
Ndanda FC 1- 0 Mtibwa Sugar
Mbao FC 1-1 Ruvu Shooting
Imeandaliwa na Rahim Mohamed