Kufuzu CHAN: Stars Yashindwa Kutamba Nyumbani Dhidi Ya Sudan

23rd September 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Taifa Stars imejiweka katika mazingira magumu ya kufuzu fainali za CHAN ambazo zinahusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani baada ya kufungwa bao 1-0 na Sudan.

Tanzania vs Sudan
Tanzania vs Sudan
SUMMARY

Matokeo hayo yanaiweka Tanzania katika wakati mgumu kwani watalazimika kushida ugenini kuanzia mabao mawili na kuendelea.

Bao pekee la Sudan limefungwa na mshambuliaji Yasir Mohamed kwenye dakika ya  61 akimalizia krosi nzuri ya Ramadhan Shareif.

Kwa matokeo hayo ni kama Sudan wameanza kulipa kisasi kwani mwaka 2011 wakati wa mechi kama hii Stars walishinda mechi zote mbili na kufuzu kwenye michuano hiyo iliyofanyika nchini Morocco. 

Stars walionekana kutawala muda mwingi wa mchezo lakini walishindwa kuvunja ngome imara ya Sudan iliyokuwa imejipanga kwa kucheza mchezo wa kujilinda na kushambulia kwa malengo.

Huo ni mchezo wa tano kwa kocha Etiene Ndayiragije kushindwa kuondoka na ushindi ndani ya dakika tisini na leo akishuhudia timu ikizamishwa ndani ya uwanja wa nyumbani.

Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo unatarajiwa kufanyika nchini Uganda, Oktoba 18 mwaka huu. Mshindi wa michezo yote miwili atafanikiwa kufuzu kwenye CHAN nchini Cameroon.

Upotevu Wa Nafasi

Mshambuliaji Shaban Chilunda, ndio atakayejilaumu zaidi baada ya kupata nafasi nyingi za kufunga lakini alishindwa kuzitumia ipasavyo huku kipa wa Sudan, Ali Aboeshren akiibuka nyota wa mchezo kwa kuokoa michomo mingi langoni mwake.

Kipindi cha kwaza Sudan walionyesha kuzidiwa kiasi cha kipa wa Stars Juma Kaseja kudaka mpira mmoja pekee.

Kocha achelewa kufanya mabadiliko

Katika mchezo wa leo kocha Ndayiragije, amelalamikiwa kwa kushidwa kufaya mabadiliko mapema wakati baadhi ya wachezaji wakioekana kuhitaji mabadiliko.

Hata alipoama kufanya mabadiliko tayari muda ulikuwa umekwenda na wachezaji aliowaingiza walicheza kwa presha kutokana na timu kuwa nyuma kwa bao moja.

Mashabiki waizomea timu.

Kufutia kiwango kibovu na matokeo mashabiki waliamua kubadilika na kuwazomea wachezaji na kocha Ndayiragije, kwa madai wameshindwa kuonyesha uzalendo.

Ugumu wa mechi ya marudiano

Matokeo hayo yanaiweka Tanzania katika wakati mgumu kwani watalazimika kushida ugenini kuanzia mabao mawili na kuendelea.

Mechi hiyo itapigwa uwanja wa Namboole nchini Uganda hivyo timu zote zitakuwa ugenini lakini Tanzania inakazi ya kufanya ili kuweza kufuzu fainali hizo ambapo itakuwa ni mara ya pili kwao kama itafanikiwa.

Imeandaliwa na Rahim Mohamed