Kombe La Shirikisho Afrika: Mwinyi Zahera Awaomba Radhi Mashabiki Wa Yanga
28th October 2019
MWANZA,Tanzania- Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, amewaomba radhi mashabiki na wanachama wa timu hiyo kwa kipigo walichopata jana kutoka kwa Pyramids FC ya Misri

Zahera amesema tatizo sio yeye kwani anaweza kuondoka na kuwaachia mashabiki timu yao lakini matokeo yakaendelea kuwa mabaya. Cha msingi ni kuvumilia kipindi hiki ili kujenga timu imara ya siku zijazo.
MWANZA,Tanzania -Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, amewaomba radhi mashabiki na wanachama wa timu hiyo kwa kipigo walichopata jana kutoka kwa Pyramids FC ya Misri ukiwa ni mchezo wa kwanza wa mtoano kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Caf.
"Nimatokeo yaliyomuumiza kila mmoja wetu lakini hatupaswi kuwa a jazba, na kuwatupia lawama wachezaji au benchi la ufundi huu ni mchezo wa kwanza bado kuna dakika 90 nyingine," amesema Zahera.
Baada ya kumalizika kwa mvhezo mashabiki wa Yanga walimshambulia Zahera kwa kumrushia chupa za maji wakichukizwa na kiwango kibovu kilichoonyeshwa na timu yao na kipigo walivhokipata wakiwa nyumbani.
Akizungumza na SportPesa News, Zahera alisema walikutana na timu bora yenye maandalizi yaliyokamilika ndio maana wakapoteza mchezo lakini haimaanishi kwamba ndio wametolewa.
"Nimatokeo yaliyomuumiza kila mtu mwenye mapenzi na Yanga, nikiri kwamba tumecheza na timu bora na imara Afrika wachezaji walipambana kwa uwezo nikweli tumepoteza lakini tunayo nafasi ya kujiuliza mechi ya marudiano," alisema Zahera.
Mkongomani huyo alisema mbali na kukutana na timu bora lakini uzoefu mdogo waliokuwa nao wachezaji wake nao vimechangia kupoteza mchezo huo nyumbani.
Amesema asilimia kubwa ya wachezaji wa Pyramids wana uzoefu na mashindano hayo na wameshafika hatua mbalimbali na wengine kubeba ubingwa tofauti na wachezaji wake ambao ndio kwanza anaiunganisha timu na wengi wao hawana uzoefu na mashindano hayo.
Zahera amesema tatizo sio yeye kwani anaweza kuondoka na kuwaachia mashabiki timu yao lakini matokeo yakaendelea kuwa mabaya. Cha msingi ni kuvumilia kipindi hiki ili kujenga timu imara ya siku zijazo.
Imeandaliwa na Raheem Mohamed