Kombe La Shirikisho Afrika: Azam Wajigawa Mafungu Kuwafuata Wazimbabwe

18th September 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania -Kikosi cha Azam FC, kinatarajia kuondoka nchini Jumapili hii kuelekea nchini Zimbabwe, tayari kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Triangle United.

Azam FC
Azam FC
SUMMARY

Baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, Azam wanahitaji ushindi wa mabao zaidi ya mawili ili kuweza kusonga mbele. 

Msafara wa Azam FC utaondoka kwa mafungu matatu, la kwanza likiwa na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo litakaloongozwa na Kocha Msaidizi, Idd Nassor Cheche.

Kundi la pili la msafara huo, litaondoka Septemba 23 na wachezaji watano waliokuwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wanajiandaa na mchezo dhidi ya Sudan, wakiwa sambamba na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, ambaye ni Kocha Mkuu wa muda wa Stars.

Aidha msafara wa mwisho utakuwa na viongozi wakuu wa timu hiyo, watakaoungana na timu hiyo siku chache za mwisho jijini Bulawayo utakapopigwa mchezo huo Septemba 28 mwaka huu.

Azam FC inayotarajia kurejea mazoezini kesho Alhamisi majira ya usiku.

Baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, Azam wanahitaji ushindi wa mabao zaidi ya mawili ili kuweza kusonga mbele. 

Kipigo walichopata Aza kwenye mchezo wao wa nyumbani ni cha kwanza kwa timu hiyo kwenye michuano ya kimataifa.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya