Kombe La Shirikisho Afrika: Azam Wagaragazwa Nyumbani Na Triangle
16th September 2019
DAR ES SALAAM, Tanzania -Azam FC wameshindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani Azam Complex, baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Triangle United ya Zimbabwe huo ukiwa ni mchezo wa awali wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa matokeo hayo, Azam wanahitaji ushindi wenye utofauti wa mabao mawili yaani 2-0 au 3-1 au zaidi ili kuweza kufuzu raundi inayofuata.
Matokeo ya leo yanaiweka Azam katika mazingira magumu yakusonga mbele ambapo sasa wanalazimika kushinda ugenini katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo nchini Zimbabwe.
Ralph Kawondera ndiye aliyepeleka kilio kwa Azam baada ya kufunga bao safi dakika ya 34, akiunganisha pasi ya Russel Madamombe.
Kuingia kwa bao hilo kulionekana kuizindua Azam na kuanza kuliandama lango la Triangle United kwa kufanya mashambulizi mengi lakini mshambuliaji wake Richard Djodi na Obrey Chirwa walikosa umakini.
Kipindi cha pili Azam walikiaza kwa kasi na kuendelea kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Triangle lakini bado mambo yalikuwa magumu kwao.
Kocha Etienne Ndayiragije wa Azam alimtoa Richard Djodi na kumuingiza Shabani Chilunda, ambaye naye alicheza kwa dakika 12 kabla ya kutolewa na nafsi yake kuchukuliwa na Iddi Kipwagile.
Kukosa mabao
Kocha Ndayiragije anakazi ya kufanya kuirekebisha safu yake ya ushambuliaji kwani imeonyesha mapungufu makubwa ikiwemo kushinda kuzitumia ipasavyo nafasi wanazotengeneza.
Iddi Selemani ndio mchezajI pekee ambaye leo alionekanz kuwasumbua walinzi wa Triangle licha mashuti yake kushindwa kulenga lango.
Chirwa tokaaa!!!!
Katika mchezo wa leo mshambuliaji Obrey Chirwa alionekana kushindwa kuendana na kasi ya mchezo baada ya kupoteza nafasi nyingi zabao.
Kutokana na hilo mashabiki wa timu hiyo walikuwa wakimpigia kelele kocha wao ili aweze kumtoa lakini mchezaji huyo aliweza kumaluza dakika zote 90.
Imeandaliwa na Rahim Mohamed