Formula 1: Lewis Hamilton Njia Nyeupe Kushinda Taji Lake La Sita Ndani Ya US GP

2nd November 2019

MIAMI, Marekani -Dereva wa magari bingwa mara tano, Lewis Hamilton ameonesha kupania kushinda taji lake la sita la dunia msimu huu baada ya kufanya vizuri kwenye mazoezi ya mwisho kabla ya US GP

Lewis Hamilton
Lewis Hamilton
SUMMARY

Hamilton ambaye ni raia wa Uingereza amejipanga kushinda taji la sita msimu huu siku ya Jumapili na anachotakiwa kufanya ni kumaliza ndani ya nane bora ili aweze kushinda taji la dunia ambalo linatolewa kwa madereva waliofanya vizuri kuliko wengine kwa msimu husika.

MIAMI, Marekani -Dereva wa magari bingwa mara tano, Lewis Hamilton ameonesha kupania kushinda taji lake la sita la dunia msimu huu baada ya kufanya vizuri kwenye mazoezi ya mwisho kabla ya US GP inayotarajia kufanyika siku ya Jumapili.

Hamilton ambaye yupo chini ya kampuni ya Mercedes alimshinda Charles Leclerc wa Ferrari kwa sekunde 0.301 huku dereva wa Red Bull, Max Verstappen akishika nafasi ya tatu.

Sebastian Vettel ameangukia nafasi ya nne akiwa na tofauti ya sekundi 0.357 wakti wa Valtteri Bottas akimaliza nafasi ya tano 0.813 nyuma ya Hamilton.

Hamilton ambaye ni raia wa Uingereza amejipanga kushinda taji la sita msimu huu siku ya Jumapili na anachotakiwa kufanya ni kumaliza ndani ya nane bora ili aweze kushinda taji la dunia ambalo linatolewa kwa madereva waliofanya vizuri kuliko wengine kwa msimu husika.

Mercedes wao wameshashinda taji mapema tangu kwenye Russia GP ambapo dereva wao Bottas aliibuka kidedea. Taji la Mercedes linahusu kampuni tu ambazo zinamiliki madereva hao wa langa langa.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya