Formula 1: Japan GP Ipo Kwenye Hatihati Ya Kutokufanyika Kutokana Na Kimbunga

10th October 2019

TOKYO, Japan -Mamlaka zinazosimamia ligi ya mashindano ya magari maarufu Formula 1 zimesema kuwa zinakusudia kusitisha Japan GP iliyopangwa kufanyika wikiendi hii kutokana na tishio la kimbunga kikali kinachoweza kuikumba nchi ya Japan.

Formula 1
Formula 1
SUMMARY

Tayari madereva kadhaa wameanza kuingia na wasiwasi kuhusu hali hiyo ambapo dereva wa Ferrari, Charles Leclerc amesema kama hali itakuwa ni ya upepo mkali na kimbunga basi hakutakuwa na namna yeyote ya wao kushiriki kwenye mbio.

TOKYO, Japan -Mamlaka zinazosimamia ligi ya mashindano ya magari maarufu Formula 1 zimesema kuwa zinakusudia kusitisha Japan GP iliyopangwa kufanyika wikiendi hii kutokana na tishio la kimbunga kikali kinachoweza kuikumba nchi ya Japan.

Kimbunga hicho kinatarajiwa siku ya Jumamosi kwenye maeneo ya Suzuka siku ambayo pia madereva watakuwa kwenye mazoezi ya mwisho kabla ya mashindano yaliyopangwa kufanyika siku ya Jumapili kwenye eneo hilo.

Taarifa kutoka Formula 1, zimesema kuwa zinafanyika jitihada kubwa kuhakikisha wanapunguza madhara ya kimbunga hicho lakini hata hivyo usalama wa madereva na mashabiki ni kipaumbele chao namba moja.

Taarifa hiyo imeendelea kwa kusema kuwa wanafuatilia kwa karibu hali hiyo na kujua ni kiasi gani pengine itakuwa na madhara kwenye Japan GP na kwamba watakuja na taarifa kamili kabla ya kuisha siku ya Ijumaa.

"Tunafuatilia kwa karibu hali ya hewa iliyopo kwasasa na kabla ya kuisha Ijumaa tutakuwa na jibu la aidha tuendelee au tusiendelee na mashindano," imesomeka taarifa hiyo.

Tayari madereva kadhaa wameanza kuingia na wasiwasi kuhusu hali hiyo ambapo dereva wa Ferrari, Charles Leclerc amesema kama hali itakuwa ni ya upepo mkali na kimbunga basi hakutakuwa na namna yeyote ya wao kushiriki kwenye mbio.

Kimbunga hicho tayari kimeshaleta mtafaruku kwenye anga la michezo ya kombe la dunia la rugby.

Imeandaliwa Na Badrudin Yahaya