Davis Cup: Mabingwa Watetezi Croatia Wapigwa 3-0 Na Urusi Kwenye Mechi Ya Kwanza
19th November 2019
MADRID, Hispania- Mabingwa watetezi wa michuano ya tenesi "Davis Cup" wameanza kvibaya kwa kupokea kipigo cha 3-0 mbele ya timu ya taifa ya Urusi.
Tofauti na michuano mingine ya tennis tuliyoizoea. Kwenye michuano ya Davis Cup timu inapata ushindi wa idadi ya mabao kama kwenye mpira wa miguu na ndiyo maana unaona timu imefungwa 2-1 nyingine 3-0.
Borna Gojo alifungwa kwa seti 6-3 6-3 na Andery Rublev na Borna Coric naye amefungwa kwa seti 6-7 (4-7) 6-4 6-4 dhidi ya Karen Khachanov na kufanya matokeo kuwa 2-0.
Wachezaji hao walipojiunga kuwa wawili kila upande, Croatia walifungwa tena na kufanya matokeo kuwa ni 3-0.
Kwenye mchezo wa kundi F, Wachezaji wa Canada, Vasek Pospisil na Denis Shapovalov wote walishinda mechi zao dhidi ya wachezaji wa Italia lakini walifungwa kwenye mechi ya wawili kwa wawili na hivyo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-1.
Pospisil yeye alimfunga Fabio Fognini kwa seti 7-6 (7-5) 7-5 na Shapovalov akimtandika Matteo Berrettin kwa seti 7-6 (7-5) 6-7 (3-7) 7-6 (7-5) na kufanya matokeo ya awali kuwa 2-0.
Waitalia walipojiunga wawili waliweza kuwafunga Wacanada hao ambao nao walicheza wawili.
Michuano hii imeanza siku ya Jumatatu ambao jumla ya mataifa 18 yanashiriki yakiwa yamepangwa kwenye makundi 6.
Kundi A Kuna: Ufaransa, Serbia, Japan.
Kundi B Kuna: Croatia, Hispania, Urusi
Kundi C Kuna: Argentina, Ujerumani, Chile
Kundi D Kuna: Ubelgiji, Australia, Colombia
Kundi E Kuna: Uingereza, Kazakhastan, Uholanzi
Kundi F Kuna: USA, Italia, Canada
Baadhi ya wachezaji nyota wanaoshiriki ni pamoja na Rafaael Nadal (Hispania), Novak Djokovic (Serbia), Matteo Berrettin (Italia) ambao hawa wote wametoka kwenye michuano ya ATP iliyoisha Jumapili iliyopita.
Wengine ni Roberto Bautista (Hispania), Gael Monfils (Ufaransa), David Goffin (Ubelgiji), Fabio Fognini (Italia), Diego Schwartzman (Argentina), Denis Shapovalov (Canada), Keren Khachanov (Urusi) na Alex de Minaur (Australia).
Utaratibu Upoje
Tofauti na michuano mingine ya tennis tuliyoizoea. Kwenye michuano ya Davis Cup timu inapata ushindi wa idadi ya mabao kama kwenye mpira wa miguu na ndiyo maana unaona timu imefungwa 2-1 nyingine 3-0.
Ushindi huo unapatika baada ya kila timu kuwa na wachezaji wawili uwanjani kwenye mechi usiku. Hatua ya kwanza mchezaji mmoja wa taifa moja anacheza mechi na mchezaji wa taifa lingine alafu mtu anayeshinda timu yake inahesabika imefunga bao la kwanza.
Unakuja mchezo wapili kwa wachezaji wale wawili ambao nao wanacheza mechi ya na anayeshida maana anaipa bao timu yake.
Baada ya hapo inakuja mechi ya mchanganyiko ambapo wachezaji wawili wa timu A wanacheza na wachezaji wawili wa timu B. Na baada ya mechi hiyo matokeo kamili yanakuwa yamepatikana.
Imeandaliwa na Badrudin Yahaya