Azam Yaondoshwa Kwenye Michuano Ya Kimataifa Baada Ya Kipigo Cha 1-0 Ugenini
28th September 2019
BULAWAYO, Zimbabwe -Licha ya kupambana kwa hali na mali kujaribu kupindua matokeo lakini kazi haikuwa rahisi kwa Azam ambao wamekubali kipigo kingine cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya Triangle na kuondolewa kwenye michuano ya shirikisho Afrika.
Kwenye mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki takribani 50 jukwaani, Azam waliweza kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga kupitia kwa washambuliaji wao Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Idd Seleman lakini walishindwa kuzitumia nafasi hizo.
Azam walikuwa wanahitaji kupata ushindi wa mabao zaidi ya mawili kufuatia kufungwa kwenye mchezo wao wa kwanza uliofanyika jijini Dar es salaam wiki mbili zilizopita lakini walijikuta wakibanwa vizuri na wenyeji wao kishaa wakaruhusu bao lililohitimisha safari yao.
Kwenye mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki takribani 50 jukwaani, Azam waliweza kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga kupitia kwa washambuliaji wao Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Idd Seleman lakini walishindwa kuzitumia nafasi hizo.
Kocha wa kikosi hicho cha Azam, Etien Ndayiragije sasa atahamishia nguvu zake zote kwenye michuano ya ligi kuu Tanzania Bara na kombe la FA kama watahitaji kurudi tena kwenye michuano hiyo msimu ujao.
Imeandaliwa na Rahim Mohamed