ATP: Rafael Nadal Aanza Kwa Kipigo Kutoka Kwa Bingwa Mtetezi Alexander Zverev

12th November 2019

LONDON, Uingereza- Mchezaji tenesi namba moja kwa ubora duniani upande wa wanaume, Rafael Nadal amepokea kichapo kutoka kwa Alexander Zverev kwenye mchezo wa kwanza tu wa michuano ya nane bora.

Raphael Nadal
Raphael Nadal
SUMMARY

Nadal ataweza kupoteza hadhi yake ya namba moja kwa ubora duniani endapo atashindwa kufika walau nusu fainali ya michuano hii na nafasi yake itachukuliwa na Novak Djokovic ambaye yeye alianza vizuri kwa ushindi hiyo jana kwenye mechi za kundi A.

LONDON, Uingereza -Mchezaji tenesi namba moja kwa ubora duniani upande wa wanaume, Rafael Nadal amepokea kichapo kutoka kwa Alexander Zverev kwenye mchezo wa kwanza tu wa michuano ya nane bora.

Mchezo huo wa kundi B ulishuhudia Nadal raia wa Hispania akikubali kufungwa kwa seti 6-2 6-4 dhidi ya Zverev ambaye ndiyo bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

Nadal ambaye hakushiriki mashindano yeyote tangu mwezi Septemba wakati a US Open amefanya makosa mengi kwenye mechi hiyo ambayo moja kwa moja yalimgharimu.

Kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo, Stefanos Tsitsipas amemfunga Daniil Medvedev kwenye mechi ambayo iliwakutanisha wachezaji wawili ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hii.

Nadal ataweza kupoteza hadhi yake ya namba moja kwa ubora duniani endapo atashindwa kufika walau nusu fainali ya michuano hii na nafasi yake itachukuliwa na Novak Djokovic ambaye yeye alianza vizuri kwa ushindi hiyo jana kwenye mechi za kundi A.

"Sikuwa vizuri kwenye mchezo huu, sina sababu yeyote nyingine wala majeruhi yangu yaliyopita siyo sababu ya mimi kufungwa," amesema Nadal mara baada ya mchezo.

Michuano hii inashirikisha wachezaji wa nafasi nane za ubora duniani ambao wanagawanywa kwenye makundi mawili. Washindi wawili wa kila kundi wanapata nafasi ya kuingia nusu fainali.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya