Scola Katusua; Bi Scolastica Akabidhiwa Hundi Baada Ya Kushinda SportPesa Jackpot Ya Tsh 260,319,980

2nd October 2019 - by Adam Mbwana

DAR ES SALAAM, Tanzania -Mkazi wa jiji la Dar es Salaam ambaye mwishoni mwa wiki aliibuka mshindi wa Jackpot ya SportPesa ya kitita cha zaidi ya Tshs milioni 260, leo amekabidhiwa zawadi yake

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Bwana Tarimba Abbas (kulia) akikabidhia hundi ya Tsh 260,319,980 kwa mshindi wa Jackpot Bi Scolastika Ngwalueson nyumbani kwake maeneo ya Mbagala Chamanzi jijini Dar es Salaam. (Picha na SportPesa News)
SUMMARY

“Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya SportPesa kwani imeweza kubadilisha maisha yangu.

"Mimi nafanya biashara ya kuuza mihogo ili kuendesha maisha lakini sasa nitafanya biashara ambayo angalau itakuwa na uwezo wa kunilipa vizuri, alisema.

DAR ES SALAAM, Tanzania -Mkazi wa jiji la Dar es Salaam ambaye mwishoni mwa wiki aliibuka mshindi wa Jackpot ya SportPesa ya kitita cha zaidi ya Tshs milioni 260, leo amekabidhiwa zawadi yake kwenye hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwake Mbagala Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Scolastika mwenye umri wa miaka 28, amejishindia kiasi hicho cha Tsh 260,319,980 milioni baada ya kubashiri mechi 13 kwa usahihi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya kiasi hicho, Ngulueson alisema kuwa alianza kubashiri SportPesa takribani mwezi mmoja na nusu uliopita na alipata hamasa zaidi baada ya kuona washindi wa jackpot wa kitita cha Milioni 825.

‘Nilianza mchezo huu wa kubashiri mwezi mmoja na nusu uliopita na kwa wiki iliyopita niliweka mikeka mitatu ya shilingi elfu mbili na mkeka mmoja ukafanikiwa.


Wachezaji Juma Mahadhi wa Yanga (kushoto) na Mzamiru Yassin wa Simba (kulia) wakikabidhi hundi ya Tsh 260,319,980 kwa mshindi wa SportPesa Jackpot bi Scolastika Ngwalueson nyumbani kwake maeneo ya Chamanzi jijini Dar es Salaam. (Picha na SportPesa News)

Kaka hunisaidia

"Hata hivyo, kulingana na kutokujua vizuri mpira wa miguu, huwa nabashiri nikisaidiwa na kaka yangu ambaye ni mpenzi sana wa mpira na leo nimeambatana naye hapa," alisema Scolastika huku akimtazama kaka yake.

“Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya SportPesa kwani imeweza kubadilisha maisha yangu.

"Mimi nafanya biashara ya kuuza mihogo ili kuendesha maisha lakini sasa nitafanya biashara ambayo angalau itakuwa na uwezo wa kunilipa vizuri, alisema.

Bila kuangalia mazingira

Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi mfano huo wa hundi, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Bwana Tarimba Abbas aliwapongeza kwa ushindi huo.

“SportPesa tunatoa zawadi kwa kila mshindi wetu ambaye ameshinda bila kuangalia mazingira anayotokea ilimradi awe na umri kuanzia miaka kumi na nane.

"Napenda kuwashukuru washindi wetu wa wiki hii na kuwaomba watumie vyema pesa walizojishindia kwa ajili ya kuendeleza maisha yao.

“Tunajivunia sana kwa kuendelea kutengeneza mamilionea wapya kila siku kwani sio Jackpot tu hata huduma zetu nyingine ambapo mbali na washindi wa Jackpot wiki hii tumetoa bonasi ya washindi waliobashiri kwa usahihi mechi kuanzia 10 hadi 12.