NBA: James Harden Afanya Balaa Lingine Rockets Wakishinda Mechi Ya Saba Mfululizo

17th November 2019 - by Adam Mbwana

HOUSTON, Marekani- James Harden amefunga vikapu 49 na kuiwezesha timu yake kuiwezesha timu yake ya Houston Rockets kuibuka na ushindi wa vikapu 125-105 dhidi ya timu ya Minnesota Timberwolves.

James Harden
SUMMARY

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Rockets walikuwa juu kwa tofauti ya alama 11 tu lakini wachezaji wa Timberwolves walishindwa kabisa kuendana na kasi ya Harden kitu kilichosababisha mchezaji huyo kutawala kwa kiasi kikubwa.

Huu ni ushindi wa saba mfululizo kwa timu ya Rockets lakini pia ni mara ya tano kwa Harden kuweza kufunga zaidi ya vikapu 40 ndani ya mechi moja msimu huu.

Mchezaji mwingine wa Rockets aliyemfuata Harden kwa kufunga vikapu vingi kwenye mchezo huo ni Ben McLemore ambaye amefunga alama 21. Austin Rivers na Chris Clemons wao wamefunga alama 19 kila mmoja.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Rockets walikuwa juu kwa tofauti ya alama 11 tu lakini wachezaji wa Timberwolves walishindwa kabisa kuendana na kasi ya Harden kitu kilichosababisha mchezaji huyo kutawala kwa kiasi kikubwa.

Karl-Anthony Towns alifunga alama 278 na kufanga rebound 27 kwa upande wa Timberwolves huku Jake Layman akifunga alama 21 kwenye mchezo huo.

LA Clippers Warudi Kwa Kasi

Baada ya kuyumba kwa kiwango chao kitu kilichofanya wapoteze michezo miwili iliyopita, hatimaye kikosi cha LA Clippers kimerudi na kasi yake ya awali na safari hii wakifanya mauaji ya kutisha kwa kuibuka na ushindi wa 101-150 dhidi ya Atlanta Hawks.

Shujaa wa mchezo huo alikuwa ni mchezaji wao mpya Paul George ambaye amefunga alama 37 ndani ya dakika 20 tu za mchezo huo.

George amecheza leo kwenye kikosi hicho ikiwa ni kwa mara ya pili tangu asajiliwe ambapo alijiunga na timu hiyo mwanzo wa msimu huku akiwa majeruhi.

Kwenye mchezo wake wa kwanza alicheza juzi na ambapo alifunga alama 33 lakini hakuweza kuikoa timu yake na kipigo kutoka kwa New Orleans Pelicans.

Hata hivyo kwenye mchezo wa leo aliweza kuziba vyema nafasi ya Kawhi Leonard ambaye hakuwa sehemu ya kikosi chao.

Lou Williams naye alifunga alama 25 akitokea benchi, huku Jerome Robinson akifunga alama 21 na Montrezl Harrell akifunga 17.

Matokeo Mengine

Houston Rockets 125-105 Minnesota Timberwolves

Milwaukee Bucks 102-83 Indiana Pacers

Atlanta Hawks 101-150 Los Angeles Clippers

Toronto Raptors 102-110 Dallas Mavericks

Brooklyn Nets 117-111 Chicago Bulls

New Orleans Pelicans 94-109 Miami Heat

Portland Trail Blazers 121-116 San Antonio Spurs

Charlotte Hornets 103-102 New York Knicks

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya