NBA: Boston Celtic Wawatandika GSW Na Kufikisha Ushindi Wa 10 Mfululizo

16th November 2019 - by Adam Mbwana

BOSTON, Marekani- Hali imeendelea kuwa nzuri kwa timu ya Boston Celtic baada ya hii leo tena kuibuka na ushindi wa vikapu 105-100 dhidi ya timu inayoangamia ya Golden State Warriors.

Boston Celtics
SUMMARY

Warriors walionekana kuwadhibiti vizuri Celtic hasa kwenye hatua za awali kabla ya kuanza kupoteana kwenye robo za kuelekea mwishoni.

Ushindi huu ni wa 10 mfululizo huku hiki kikiwa ni kipigo cha 10 kati ya mechi 12 walizocheza Golden State Warriors msimu huu.

Jayson Tatum alikuwa ni nyota wa mchezo akimaliza na vikapu 24 ambavyo vilikuwa ni vingi ukilinganisha na wachezaji wengine kwenye mchezo huo.

Brown yeye alimaliza na vikapu 22 wakati Kemba Walker akifunga vikapu 20. Marcu Smart alikuwa nafasi ya nne kwa waliofunga vikapu vingi upande wa Celtic akifunga vikapu 15.

Warriors walionekana kuwadhibiti vizuri Celtic hasa kwenye hatua za awali kabla ya kuanza kupoteana kwenye robo za kuelekea mwishoni.

Kwenye mchezo huo Warriors waliweza kumkaribisha tena kikosini nyota wa Draymond Green ambaye alikosekana kwenye mechi kadhaa kwasababu ya majeraha.

Hata hivyo bado wanakosa huduma ya mchezaji wao nyota zaidi Stephen Curry aliyevunjika mkono kwenye mechi za awali na Klay Thompson ambaye yeye ni majeruhi wa muda mrefu.

Matokeo Mengine:

Boston Celtics 105-100 Golden State Warriors

Sacramento Kings 97-99 Los Angeles Lakers

Philadelphia 76ers 119-127 Oklahoma City Thunder (OT)

Indiana Pacers 102-111 Houston Rockets

Utah Jazz 106-107 Memphis Grizzlies

Detroit Pistons 106-109 Charlotte Hornets

Washington Wizards 137-116 Minnesota Timberwolves

San Antonio Spurs 109-111 Orlando Magic

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya