Ligi Kuu Bara: Simba Hawakamatiki, Kagera Sugar Wakikwaa Kisiki Kingine

30th September 2019 - by Adam Mbwana

MARA, Tanzania -Klabu ya Simba imeendelea kujikusanyia point tatu muhimu baada ya hii leo kufanikiwa kuwafunga Biashara United ya Mara kwa jumla ya mabao 2-0 kwenye mchezo uliofanyika kwenye dimba la Karume.

Simba
SUMMARY

Nayo klabu ya Kagera Sugar ambayo ilianza ligi ya msimu huu kwa kishindo baada ya kushinda mechi zao tatu za kwanza, wamejikuta wakifungwa tena leo na JKT Tanzania kwa bao 1-0 ikiwa ni siku mbili tu tangu walipofungwa na Simba. Bao la JKT Tanzania limefungwa na Hassan Mwaterema.

Washambuliaji Meddie Kagere na Miraj Athumani ndio waliofunga mabao yote mawili hayo ambayo yamezidi kuwasogeza Simba kileleni baada ya kushinda michezo yao yote minne waliyocheza msimu huu.

Biashara ambao wiki iliyopita wamemtimua kocha wao Amri Said bado wanaendelea kusaka ushindi wao kwanza ikiwa tayari wameshashuka dimbani mara tano na wakiwa wameambulia alama mooja tu.

Nayo klabu ya Kagera Sugar ambayo ilianza ligi ya msimu huu kwa kishindo baada ya kushinda mechi zao tatu za kwanza, wamejikuta wakifungwa tena leo na JKT Tanzania kwa bao 1-0 ikiwa ni siku mbili tu tangu walipofungwa na Simba. Bao la JKT Tanzania limefungwa na Hassan Mwaterema.

Huo unakuwa ni mchezo wa pili kwa Kagera kupoteza mfululizo kwenye uwanja wao wa nyumbani baada ya kushinda mechi zao tatu mfululizo za ugenini.

Mtibwa Sugar kwa upande wao bado wanajikongoja baada ya hii leo kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani walipokuwa wakicheza dhidi ya Mbeya City. Kiungo wa Mtibwa, Abdulhalim Humud ndiyo alikuwa wakwanza kufunga bao kabla ya Peter Mapunda kusawazisha kwa upande wa Mbeya City.

Matokeo hayo yanawaacha Mtibwa wakiwa na alama mbili tu katika michezo mitano ambayo wameshuka dimbani msimu huu.

Kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, KMC wamebanwa mbavu na Ndanda baada ya kufungana bao 1-1. Ally Ramadhan alikuwa wa kwanza kufunga bao kwa upande wa wenyeji KMC lakini Salum Chubi akasawazisha kipindi cha pili.

Matokeo mengine ya sare yalikuwa huko Iringa kwenye uwanja wa Samora, ambapo wenyeji Lipuli wamelazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Tanzania Prison. 


Imeandaliwa na Rahim Mohamed