EPL: Chelsea Wakumbana na Kipigo Darajani Kutoka Kwa West Ham, Man City Wakikabwa Koo Ugenini

1st December 2019 - by Adam Mbwana

LONDON, Uingereza- Klabu ya Chelsea wameshindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani wa Stamford Bridge baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa majirani zao timu ya West Ham United kwenye "London Derby".

Chelsea FC
SUMMARY

Licha ya kushinda mchezo huo lakini West Ham wanapaswa kumpa hongera mlinda lango wao David Martin aliyekuwa kizingiti dhidi ya mashambulizi ya Chelsea yaliyokuwa yanafanyika mfululizo hadi mwisho wa mchezo.

Bao la West Ham kwenye mchezo huo limefungwa na mlinzi Aaron Cresswell dakika tatu baada ya mapumziko na kupunguza presha kidogo kwa kocha Manuel Pellegrini ambaye hajashinda kwenye michezo nane iliyopita.

Ushindi ndani ya Stamford Bridge ni wa kwanza kwa West Ham baada ya miaka 17 na umewafanya kufikisha alama 16 baada ya kushuka dimbani mara 14.

Licha ya kushinda mchezo huo lakini West Ham wanapaswa kumpa hongera mlinda lango wao David Martin aliyekuwa kizingiti dhidi ya mashambulizi ya Chelsea yaliyokuwa yanafanyika mfululizo hadi mwisho wa mchezo.

Man City Wakabwa Koo

Man City nao wakiwa ugenini wamejikuta wakizidi kudondosha pointi baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na timu ya Newcastle United.

Bao la dakika za mwisho la kiungo wa zamani wa Liverpool, Jonjo Shelvey ndiyo lililokatisha matumaini ya Man City kuzoa alama tatu za ugenini.

Man City kwenye mchezo huo ndiyo walikuwa wa kwanza kufunga bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Raheem Sterling lakini bao hilo halikudumu zaidi ya dakika tatu kabla ya kuchomolewa na Jetro Willems.

Kipindi cha pili tena Man City walitafuta bao kwa nguvu na walifanikiwa kufunga kupitia Kevin De Bruyne kwenye dakika ya 82. Wakati wakijua tayari alama zote tatu ni zao ndipo Shelvey alipochomoa betri na kuwafanya kuzidi kupotez matumaini ya kutetea taji lao.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya