ATP: Rafael Nadal Amtangazia Kiama Novac Djokovic Kwenye Nafasi Ya Kwanza
9th November 2019
LONDON, Uingereza- Mchezaji wa tenesi, Rafael Nadal raia wa Hispania amesema kuwa yupo fiti kuianza michuano ya nane bora ya dunia (ATP) na kupambana dhidi ya Novak Djokovic kuwania nafasi ya kwanza kwa ubora duniani.
Michuano ya ATP ni ya kumalizia msimu wa mchezo wa tenisi ambapo wachezaji nane kwa ubora duniani wanagawanywa kwenye makundi mawili na wanacheza mechi tatu kila mmoja huku walioshika nafasi mbili za juu wanakwenda nusu fainali.
Nadal anashika nafasi ya kwanza kwa ubora kwasasa lakini anaweza akimaliza mwaka akiwa chini endapo atashindwa walau kufika nusu fainali kwenye michuano hii ambayo ina upinzani wa aina yake.
Kama unakumbuka ni kwamba Nadal alijiondoa kwenye michuano ya Paris Masters iliyofika tamati wiki iliyopita na lengo lake ilikuwa ni kujipa muda zaidi wa kujiandaa na michuano ya ATP ambayo inafanyika London kuanzia kesho Jumapili.
"Ni michuano migumu kwasababu unaanza kukutana na wachezaji wakubwa kuanzia mwanzo tu wa michuano hivyo cha msingi ni kuwa fiti asilimia 100 tangu mwanzo wa mashindano,' amesema mshindi huyo mara 19 wa Grand Slams.
Msimu uliopita Nadal alikosa fursa ya kushiriki michuano hii kutokana na majeruhi ya goti yaliyokuwa yanamsumbua.
Michuano ya ATP ni ya kumalizia msimu wa mchezo wa tenisi ambapo wachezaji nane kwa ubora duniani wanagawanywa kwenye makundi mawili na wanacheza mechi tatu kila mmoja huku walioshika nafasi mbili za juu wanakwenda nusu fainali.
Nadal yupo kundi A ambalo linamjumuisha pamoja na Daniil Medvedev, Stefanos Tsitsipas, Alexander Zverev.
Kundi B lina Rodger Federer, Novak Djokovic, Dominic Thiem na Matteo Berrettin.
Imeandaliwa na Badrudin Yahaya