"Kwa Wanaotaka Kuwa Mamilionea Basi Mpango Mzima Ni SportPesa," Mshindi Wa Jackpot Bonus Afunguka

18th September 2019 - by Adam Mbwana

DAR ES SALAAM, Tanzania- Je umeshawahi kukatishwa tamaa na watu wako wa karibu unaowaamini kiasi kwamba ukavunjika moyo lakini ukayashinda majaribu kisha ukafanikiwa kupindua meza kibabe?

Mshindi wa Jackpot Bonus, Jumanne Ramadhani (kushoto) akikabidhiwa mfano wa hundi ya Tsh 17,771,715/= na meneja mahusiano wa SportPesa, Bi Sabrina Msuya katika ofisi za SportPesa jijini Dar es Salaam. (Picha na SP News)
SUMMARY

"Tumeona kampuni nyingi za masuala ya kubashiri lakini niwe muwazi kwa kusema kuwa kampuni ya SportPesa ni bora kabisa kuliko zote Afrika Mashariki, kauli hii naitoa kutoka moyoni,? amesema Ngula.

Hilo sio jambo geni kwenye maisha yetu ya kila siku kwani kuna watu wamekuwa hawaamini sana kwenye baadhi ya njia ambazo tunapita ili kufanikisha baadhi ya mambo na malengo yetu tuliyojpangia.

Kama Jumanne Ramadhan Ngula angekuwa ni mtu wa kuyumbishwa basi nakwambia leo hii ninavyozungumza na wewe asingekuwa milionea mpya hapa mjini.

Dereva huyo wa bodaboda ni mshindi wa bonasi ya shilingi milioni 17,771,715 kutoka kwenye Jackpoti ya SportPesa baada ya kufanikiwa kubashiri mechi 12 kati ya 13 mapema wiki hii.

Safari yake hadi kufikia ushindi huo wa donge nono la fedha haikuwa rahisi kwani ilibidi ashinde vijembe vya mkewe ambaye alikuwa haamini kabisa kile anachofanya mumewe na mara kadhaa alikuwa akiona kama anapoteza muda.

Anapoteza muda?

Jumanne Ngula sasa ni milionea na mkewe huyo kwasasa atakuwa anachekea pembeni huku akiwa na utitiri wa mipango ambayo angependa kufanya na mumewe kuhusu fedha hizo zilizotinga ndani ya familia yao.

"Wakati nikiwa nacheza mke wangu alikuwa haamini kabisa haya mambo na mara kadhaa aliniambia niachane nayo, hata nilipomuonesha meseji ya ushindi bado alikataa kuamini hadi azione hela nyumbani," amesema Ngula huku akiwa na tabasamu la kimilionea.

SportPesa Ni Kampuni Bora

Jumanne Ngula anasema kuwa kuna kampuni nyingi ambazo zinafanya michezo ya ubashiri lakini kati ya hizo zote SportPesa ni bora kuliko zote Afrika Mashariki.

"Tumeona kampuni nyingi za masuala ya kubashiri lakini niwe muwazi kwa kusema kuwa kampuni ya SportPesa ni bora kabisa kuliko zote Afrika Mashariki, kauli hii naitoa kutoka moyoni,? amesema Ngula.

Je Ufanyaje Ili Uwe Milionea?

Jumanne Ramadhan Ngula anawaambia watu wote wanaotaka kuwa mamilionea hapa nchini wasihangaike wala wasiwe na wasiwasi kwani kampuni ya SportPesa pekee ndiyo inaweza kuwafanya kutimiza malengo hayo.

"Kwa wale ambao wanataka kuwa mamilionea, ambao wanahitaji pesa ndefu, mpango mzima ni SportPesa," amemalizia Ngula.

Jackpot Mpya

Bado una nafasi ya kuwa MILIONEA wiki hii kama ilivyokuwa kwa Jumanne Ramadhani. Jackpot ya SportPesa wiki hii inasoma Tsh 243,520,580. 

Bofya Hapa kucheza Jackpot ya mechi 13 ili uwe Milionea na ukipatia mechi 10, 11, 12 kuna Bonus za kukata na shoka.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya