Tetesi: Charles Mkwasa Ataja Maeneo Matatu Yenye Mapungufu Kikosi Cha Yanga

12th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Kaimu kocha mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kuwa kikosi hicho kinamapungufu kwenye maeneo matatu muhimu ambayo angependa kuona yakifanyiwa kazi kwenye dirisha dogo la usajili.

Charles Boniface Mkwasa
Charles Boniface Mkwasa
SUMMARY

"Mimi bado siyo kucha wa muda mrefu kwahiyo siwezi kupendekeza majina lakini kwa nilivyoiona timu hii tangu mwanzo wa msimu nimegundua mapungufu kidogo kwenye maeneo hayo," amesema Mkwasa.

DAR ES SALAAM, Tanzania- Kaimu kocha mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kuwa kikosi hicho kinamapungufu kwenye maeneo matatu muhimu ambayo angependa kuona yakifanyiwa kazi kwenye dirisha dogo la usajili.

Mkwasa ameyataja maeneo hayo kuwa ni upande wa ulinzi wa kushoto, kiungo wa ushambuliaji na mshambuliaji mmoja.

Akizungumza na SportPesa News, Mkwasa amesema kuwa kama viongozi wa timu ya Yanga wakirekebisha kwenye maeneo hayo kuna uwezekano mkubwa timu hiyo ikawa nzuri zaidi ya ilivyokuwa hivi sasa.

"Mimi bado siyo kucha wa muda mrefu kwahiyo siwezi kupendekeza majina lakini kwa nilivyoiona timu hii tangu mwanzo wa msimu nimegundua mapungufu kidogo kwenye maeneo hayo," amesema Mkwasa.

Hata hivyo Mkwasa amesema kuwa wachezaji ambao wanacheza kwenye nafasi hiyo kwasasa siyo wabaya na bado wanaweza kufanya vizuri msimu huu kama wataongeza kujituma.

Yanga wamekuwa wakihusishwa na wachezaji kadhaa kuelekea kwenye dirisha dogo la usajili linalotarajia kufunguliwa Novemba 15.

Baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na Eric Rutaga na Michael Sarpong wanaocheza Rayon Sport ya Rwanda huku pia wakihushwa na taarifa za kutaka kumrejesha kiungo wao wa zamani Haruna Niyonzima ambaye kwasasa anacheza AS Kigali baada ya kuondoka Simba mwisho wa msimu uliopita.

Eneo la ushambuliaji la Yanga linaundwa na nyota David Molinga, Juma Balinya na Maybin Kalenga ambao kwa pamoja wamefunga mabao matatu tu kwenye michuano yote tangu mwanzo wa msimu.

Mkwasa alikabidhiwa timu hiyo mapema wiki iliyopita akichukuwa nafasi ya kocha Mwinyi Zahera ambaye kibarua chake kilifika mwisho mara baada ya kuingoza timu kwenye mechi 10 msimu huu.

Kwenye mechi yake ya kwanza aliiwezesha timu kuibuka na ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Ndanda kwenye mchezo wa ligi kuu bara.

Imeandaliwa na Rahim Mohamed