Ligi Kuu Bara: Mambo Sita Yaliyojiri Kwenye Mzunguko Wa 10 Wa Ligi

11th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Ligi kuu bara inazidi kushika kasi huku miamba ikiwa inaoneshana undava viwanjani. Haya ni mambo matano makubwa yaliyojiri katika mizunguko iliyopita hivi karibuni.

Patrick Sibomana
Patrick Sibomana
SUMMARY

Unaambiwa kwenye ligi hii hakuna timu inayopenda kucheza ugenini kama Kagera Sugar msimu huu. Ndiyo! Ni kwasababu wameshinda mechi zao zote sita za ugenini huku ushindi wa mwisho wakiupata jana tu dhidi ya KMC.

DAR ES SALAAM, Tanzania -Ligi kuu bara inazidi kushika kasi huku miamba ikiwa inaoneshana undava viwanjani. Haya ni mambo matano makubwa yaliyojiri katika mizunguko iliyopita hivi karibuni.

Tanzania Prison Bado Ving'ang'anizi

Licha ya kuwa kwenye nafasi ya tatu na alama zao 19 lakini Tanzania Prison bado ndiyo timu pekee ambayo haijawahi kupoteza mchezo wowote msimu huu.

Wakiwa wameshuka dimbani mara 11 watu wengi walidhani kuwa huenda rekoid yao ingeharibiwa na Simba kwenye mechi waliyocheza Alhamis kwenye uwanja wa uhuru lakini bado vijana hao wa kocha Adolf Rishald walithubutu kupata sare ya 0-0.

Kagera Sugar Wazee Wa Ugenini

Unaambiwa kwenye ligi hii hakuna timu inayopenda kucheza ugenini kama Kagera Sugar msimu huu. Ndiyo! Ni kwasababu wameshinda mechi zao zote sita za ugenini huku ushindi wa mwisho wakiupata jana tu dhidi ya KMC.

Kwasasa wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na alama 20 baada ya kushuka dimbani mara 10.

Jackson Mayanja Hana Jipya

KMC iliyotarajiwa msimu huu siyo kabisa tunayoiona mbele yetu. Msimu uliopita chini ya kocha Etiene Ndayiragije ilikuwa moto na ikafanya usajili mkubwa kabla ya kuanza kwa msimu huu.

Watu wengi walitegemea kuona makubwa zaidi hasa baada ya kocha mzoefu wa soka la Tanzania, Mganda, Jackson Mayanja alipopewa nafasi ya kuziba pengo la Ndayiragije. Lakini hivi navyokwambia timu ipo chini ikiwa na alama 8 tu ndani ya mechi 8 na mchezo wa mwisho wamefungwa jana tu na Kagera Sugar.

Singida United Wameshakubali Yaishe?

Kipigo cha 5-1 kutoka kwa Lipuli kimeifanya Singida United kuwa timu ambayo hadi sasa ikiwa bado haijawahi kupata ushindi msimu huu. Wamecheza mechi 11 na walichoambulia ni sare nne tu huku mechi nyingine zote wakifungwa.

Hat Trick Ya Pili Ya Msimu

Baada ya Ditrim Nchimbi wa Polisi Tanzania kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat trick msimu huu, hat trick ya pili imefungwa na Daruesh Saliboko wa Lipuli.

Tofauti ni kwamba Nchimbi alifunga hat trick dhidi ya Yanga wakati Saliboko amewafunga Singida United, lakini yote kwa yote wachezaji wote hao wameweka rekodi yao msimu huu.

Kama utakubaliana na mimi ni kwamba, hakuna kitu kigumu kupatikana kwenye ligi yetu kama mabao mengi kwenye mechi moja au mchezaji mmoja kufunga mabao mengi kwenye mechi moja.

Ni mara chache sana kuona zinafungwa hat trick nyingi ndani ya msimu mmoja. Na ndio maana sio ajabu kuona ushindi wa 5-1 kwa Lipuli dhidi ya Singida United na ushindi mkubwa zaidi msimu huu.

Yanga Yapata Ushindi Mwingine Mtwara

Kama ulikuwa haujui basi nikufahamishe tu kuwa ushindi wa Yanga dhidi ya Ndanda ndani ya Nangwanda ni wa mara ya pili tu.

Tangu Ndanda walipopanda daraja mwaka 2014 wamekuwa na kawaida ya kuwakazia Yanga kwenye uwanja huo na mara kadhaa Wanajangwani hao wamekuwa wakiambulia sare tu. Hiyo ni bila kujali Ndanda wapo kwenye hali gani.

Hat hivyo ushindi wa jana unafanya kuongeza idadi na kufikia 2, mara ya mwisho walishinda hapo ilikuwa ni msimu wa 2017-18 kocha mkuu akiwa ni George Lwandamina.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya