EURO 2020: Raheem Sterling Amuanzishia Varangati Joe Gomez Kambini Uingereza

12th November 2019

LONDON, Uingereza -Wikiendi hii kulikuwa na bonge la mechi kwenye ligi kuu ya Uingereza ambapo tulishuhudia mafahari wawili Liverpool na Manchester City wakitoana jasho ndani ya dimba la Anfield.

Sterling
Sterling
SUMMARY

"Sterling ameondolewa kwenye kikosi cha Alhamisi kutokana na usumbufu alioleta kambini," imeseomeka taarifa hiyo ambayo ni maamuzi ya kocha Southgate.

LONDON, Uingereza -Wikiendi hii kulikuwa na bonge la mechi kwenye ligi kuu ya Uingereza ambapo tulishuhudia mafahari wawili Liverpool na Manchester City wakitoana jasho ndani ya dimba la Anfield.

Mbali na matokeo ya ushindi wa 3-1 ambao Liverpool waliupata lakini mchezo huo pia uligubikwa na vibweka vingi sana. Moja ya tukio lilikuwa ni kutunishiana misuli kwa wachezaji wawili raia wa Uingereza, Raheem Sterling (Man City) na Joe Gomez (Liverpool).

Tukio hilo lilitokea kwenye dakika za mwishoni na ilikuwa ni muda mfupi tu mara baada ya Gomez kuingia uwanjani kuchukuwa nafasi ya Mohamed Salah.

Kama ulikuwa unadhani kuwa tukio hilo liliishia pale uwanjani basi nikwambie tu kuwa unajidanganya. Wachezaji hao ambao wote waliitwa na kocha Gareth Southgate kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza wamekutana kambini siku ya jana na unaambiwa wameanzishiana tena vagi kama kawaida.

Taarifa ya tukio hilo kwenye kambi ya timu ya taifa imetolewa leo na FA ambapo wamesema kuwa kocha Southgate ameamua kumuondoa Sterling kwenye mipango yake kuelekea mchezo wao wa Alhamisi dhidi ya Montenegro.

"Sterling ameondolewa kwenye kikosi cha Alhamisi kutokana na usumbufu alioleta kambini," imeseomeka taarifa hiyo ambayo ni maamuzi ya kocha Southgate.

Hata hivyo taarifa hiyo ilikwenda mbali na kusema kuwa wachezaji hao kwasasa wana mawasiliano mazuri na hakuna tatizo tena.

Uingereza wanatarajia kucheza mchezo wao wa 1000 tangu timu ya taifa ya wanaume ilipoanzishwa na kama wataibuka na ushindi kwenye dimba la Wembley basi watakuwa wamekata tiketi ya kushiriki Euro 2020.

Three Lions wanaongoza kundi A wakiwa alama tatu juu ya Czech Republic na alama nne dhidi ya Kosovo ambao watacheza nao kwenye mchezo wa Jumapili ijayo.

Sterling, 24 alijunga na Man City mwaka 2015 akitokea Lverpool. Ameshacheza michezo 55 ya timu ya taifa na akifunga mabao 12 huku Gomez akiwa amecheza mechi 7.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya