EPL: Liverpool Njia Nyeupe Ubingwa Msimu Huu, Man United Mambo Safi

11th November 2019

LIVERPOOL, Uingereza- Klabu ya Liverpool imezidi kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kubeba taji msimu huu baada ya hii leo kuwachakaza Manchester City kwa mabao 3-1 na kukaa kileleni kwa tofauti ya alama 8.

Wachezaji wa Liverpool wakishangilia bao
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia bao
SUMMARY

Mchezo huo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka duniani ulianza kwa kasi na dakika ya sita tu kiungo raia wa Brazil, Fabinho alitandika mkwaju mkali uliomshinda mlinda lango Claudio Bravo na kujaa wavuni.

LIVERPOOL, Uingereza -Klabu ya Liverpool imezidi kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kubeba taji msimu huu baada ya hii leo kuwachakaza Manchester City kwa mabao 3-1 na kukaa kileleni kwa tofauti ya alama 8.

Mchezo huo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka duniani ulianza kwa kasi na dakika ya sita tu kiungo raia wa Brazil, Fabinho alitandika mkwaju mkali uliomshinda mlinda lango Claudio Bravo na kujaa wavuni.

Sekunde chache kabla ya bao hilo, Man City walidai penati ambapo ilionekana dhahiri mlinzi wa kati wa Liverpool, Alexander Anorld akiunawa mpira lakini mwamuzi Michal Olver alikataa na hakutaka hata kuhakiki kwenye VAR.

Man City walicheza kwa mfumo wao wa pasi na kutengeneza nafasi kutoka kwenye pande zote mbili yaani kulia alipokuwa Benardo Silva na kushoto alipokwepo Raheem Sterling. Hata hivyo itabidi wamlaumu Sergio Aguero ambaye alikuwa muhanga wa kukosa nafasi nyingi za kuwarudisha wenzie mchezoni.

Mohamed Salah alifunga bao la pili kwenye dakika ya 13 akiunganisha kwa kichwa krosi nzuri iliyopigwa kutoka upande wa kushoto na Andy Robertson na bao hilo lilidumu hadi mapumziko kufanya timu kwenda vyumbani matokeo yakiwa 2-0.


Dakika sita tu baada ya timu kutoka mapumziko Sadio Mane alifunga bao la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi ya nahodha wake Jordan Henderson na kuhitimisha kipigo hicho kwa City ambao ni mabingwa mara mbili mfululizo wa ligi hiyo.

Bao la kufutia machozi la Man City limefungwa na Benardo Silva kwenye dakika ya 77 ya mchezo huo.

Man City kwenye mchezo wa leo wamekosa huduma ya kipa wao Ederson ambaye aliumia kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Atalanta siku ya Jumatano. Kutokana na hilo ndipo kocha Pep Guardiola alipomuanzisha Bravo golini

Ushindi huo unawafanya Liverpool kuwa kileleni kwa tofauti ya alama 8 dhidi ya Leicester City na Chelsea ambao wamelingana pointi kwenye nafasi ya pili na ya tatu huku Man City akishuka hadi nafasi ya nne na wakiwa wameachwa alama 9.

VAR Yatia Fora

Mbali na matokeo ya mchezo huo lakini VAR itakuwa ni sehemu ya mjadala mkubwa kutokana na kushindwa kuamua matukio makubwa mawili ambayo huenda yangeinufaisha Man City kwenye mchezo huo.

Sekunde chache kabla ya bao la kwanza la Liverpool, Man City walikuwa wanashambulia na mpira uliopigwa shuti na Ilkay Gundogan ulionesha dhahiri kumgongo mkononi mlinzi wa Liverpool, Alexander Anorld.

Kama hiyo haitoshi, dakika za mwishoni mpira uliopigwa na Sterling ulionekana tena kumgonga mkononi Anorld. Matukio hayo yote mawili mwamuzi Oliver alishindwa kuyatolea uamuzi na hata VAR haikuweza kuingilia.

Man United Mambo Safi

Huko Old Trafford, Manchester United leo wamepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Brighton na kupaa hadi kwenye nafasi ya saba kwenye msimamo wa EPL.

Mabao ya Man United kwenye mchezo huo yamefungwa na Andreas Perreira na Marcus Rashford huku kiungo wa Brighton, Davy Propper akijifunga bao moja. Bao la kufutia machozi la Brighton limefungwa na mlinzi wa kati Lewis Dunk.

Ushindi huo ni wa tano kati ya mechi sita walizocheza Man United kwenye michuano yote.

Matokeo Mengine:

Wolves 2-1 Aston Villa

Imeandaliwa na Badrudin Yahay