AFCON 2021: Samatta Aahidi Makubwa Kuelekea Mechi Za Equaterial Guinea, Libya

12th November 2019

DAR ES SALAA, Tanzania- Washambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Simon Msuva wametua nchini tayari kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2021 dhidi ya Equateria Guinea mchezo uliopangwa kuchezwa Ijumaa, Uwanja wa Taifa.

Samatta
Samatta
SUMMARY

"Kwenye mechi za kufuzu zilizopita tulianza vibaya kwa kutoka sare na Leseotho kwenye uwanja wetu wa nyumbani, hali ile ilitufanya tumalize mechi za kundi kwa ugumu. Mwaka huu tunataraji kuanza vizuri tangu mwanzo ili tujihakikishie nafasi mapema," amesema Samatta ambaye pia ni nahodha wa kikosi cha Stars.

DAR ES SALAA, Tanzania -Washambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Simon Msuva wametua nchini tayari kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2021 dhidi ya Equateria Guinea mchezo uliopangwa kuchezwa Ijumaa, Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ni wa kwanza wa kuwania kufuzu kwenye michuano hiyo ambayo imepangwa kufanyika nchini Cameroon.

Samatta ambaye wiki iliyopita akiwa na timu yake ya KRC Genk alifunga bao dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya ndani ya Anfield amesema kuwa wanatarajia kuanza kwenye mechi hizi kwa kishindo kwa kupata kwanza ushindi wa nyumbani.

"Kwenye mechi za kufuzu zilizopita tulianza vibaya kwa kutoka sare na Leseotho kwenye uwanja wetu wa nyumbani, hali ile ilitufanya tumalize mechi za kundi kwa ugumu. Mwaka huu tunataraji kuanza vizuri tangu mwanzo ili tujihakikishie nafasi mapema," amesema Samatta ambaye pia ni nahodha wa kikosi cha Stars.

Samatta ametua nchini usiku wa kuamkia leo akiwa ameongozana na winga wa Stars, Msuva ambaye naye anakipiga Morocco kunako klabu ya Difaa el Jadid.

Kwa upande wake kocha wa Stars, Etiene Ndayiragije akizungumza na SportPesa News amesema kuwa timu yake imeanza vyema maandalizi yake tangu walipoingia kambini siku ya Jumamosi na kwamba wanataraji kufanya vizuri kwenye michezo miwili inayowakabili mbele yao.

"Program zangu zipo vizuri na tunafanya maandilizi ya nguvu, wachezaji wote ninao kambini isipokuwa Samatta na Msuva (wamewasili tayari) ambao nadhani usiku wa leo watakuwa wameshafika nchini," amesema Ndayiragije.

Stars inakabiliwa na michezo miwili muhimu ambapo siku ya Ijumaa watakuwa uwanjani dhidi ya Equaterial Guinea na siku nne baadaye watasafiri kuwafuata Libya kwenye mechi ya ugenini.

Mechi zote hizo ni za kundi J ambapo pia wamo wakali Tunisia. Baada ya mechi hizi mbili za awali ratiba itasimama hadi Agosti 31, 2020 ambapo Stars watakwenda ugenini kukabiliana na Tunisia.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed