AFCON 2021: Matatizo Ya Kifamilia Yamuondoa Mkude Kikosini Stars

12th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars', Eteine Ndayiragije amempa ruhusa kiungo wa Simba, Jonas Mkude ya kuondoka kambini na kwenda kushughulikia matatizo yake ya kifamilia.

Jonas Mkude
Jonas Mkude
SUMMARY

"Mkude aliomba ruhusa ya kutojiunga na kambi ili kushughulikia matatizo yake ya kifamilia, ruhusa hiyo alipewa. Amerudi tena kambini Jumatatu na kueleza kuwa bado hajamaliza matatizo yake na amepewa tena ruhusa," imesomeka taarifa hiyo ya TFF.

DAR ES SALAAM, Tanzania- Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars', Eteine Ndayiragije amempa ruhusa kiungo wa Simba, Jonas Mkude ya kuondoka kambini na kwenda kushughulikia matatizo yake ya kifamilia.

Taarifa iliyotolewa muda mfupi uliopita na TFF inasema kuwa Mkude aliomba ruhusa kwa kocha mkuu mapema kabla ya kuanza kambi siku ya Jumamosi na aliruhusiwa kuchelewa kujiunga na timu.

Hata hivyo siku ya Jumatatu, Mkude alirudi kambini na kuongea na kocha na kwambia kuwa bado hajamaliza matatizo yake na hivyo akaruhusiwa tena akashughulikie hadi yaishe.

"Mkude aliomba ruhusa ya kutojiunga na kambi ili kushughulikia matatizo yake ya kifamilia, ruhusa hiyo alipewa. Amerudi tena kambini Jumatatu na kueleza kuwa bado hajamaliza matatizo yake na amepewa tena ruhusa," imesomeka taarifa hiyo ya TFF.

Stars wapo kambini kwa ajili ya kujiwinda na michezo miwili ya kuwania kufuzu michuano ya Afcon nchini Cameroon mwaka 2021.

Mchezo wa kwanza utakuwa siku ya Ijumaa ambapo utapigwa ndani ya Uwanja wa Taifa. Siku nne baadaye Stars watasafiri kwenda nchini Libya kukabiliana na wenyeji hao kwenye mchezo wa pili wa kundi J ambapo pia Tunisia wamo ndani yake.

Mkude amekuwa ni moja kati ya nguzo muhimu kwenye idara ya kiungo tangu kocha Ndayiragije alipochukuwa mikoba ya kukinoa kikosi cha Stars kutoka kwa Emmanuel Amunike.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF ni kwamba pengo lake halitaweza kuzibwa kutokana na muda uliobaki.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya