AFCON 2021: Je Nyota Hawa Watano Wa EPL Watazibeba Nchi Zao Kimataifa?

13th November 2019

DAKAR, Senegal- Uhondo wa ligi ya Uingereza umeweka kituo kwanza ili tupishe shamrashamra za michezo ya timu za taifa.

Riyad Mahrez
Riyad Mahrez
SUMMARY

DAKAR, Senegal- Uhondo wa ligi ya Uingereza umeweka kituo kwanza ili tupishe shamrashamra za michezo ya timu za taifa.

DAKAR, Senegal -Uhondo wa ligi ya Uingereza umeweka kituo kwanza ili tupishe shamrashamra za michezo ya timu za taifa.

Kama ilivyo huko barani ulaya, timu zinawania kufuzu kucheza Euro 2020 huku kwetu barani Afrika vigogo watakuwa wakishuka dimbani kumenyana kwa ajili ya kudai nafasi za Afcon 2021 nchini Cameroon.

Wapo nyota kutoka Afrika ambao tumezoea kuwaona wakisumbua sana ndani ya ligi kuu ya Uingereza. Hata hivyo sasa ni zamu yetu kuwaona mubashara kwenye maeneo mbalimbali ndani ya bara la Afrika.

Kabla ya kufika mbali nikwambie tu kwamba kwenye wiki hii hatutaweza kumuona Mohamed Salah ambaye ameumia kwenye mchezo wa ligi uliopita wakati timu yake ya Liverpool ilipopata ushindi wa 3-1 dhidi ya Man City.

SportPesa News inakueleta nyota watano kutoka EPL ambao kwa pamoja inatupasa kuwafutilia zaidi kwenye kipindi hiki cha msimu wa tmu za taifa.

Sadio Mane (Liverpool/Senegal)

Msimu uliopita wa michuano ya Afcon, Sadio Mane pamoja na wenzake walifanikiwa kufika hadi hatua ya fainali lakini walipoteza mchezo mbele ya Algeria ambao ndiyo mabingwa hadi hivi sasa.

Hata hivyo kikosi cha Senegal bado kinaundwa na nyota wengi ambao kama wataendelea kukaza basi wanayo nafasi ya kufanya vizuri kwenye Afcon ya mwaka 2021.

Kwneye kikosi cha kuna nyota wa majina makubwa lakini wote hawawezi kumfikia Mane ambaye ni mshindi wa ligi ya mabingwa akiwa na Liverpool msimu uliopota.

DAKAR, Senegal- Uhondo wa ligi ya Uingereza umeweka kituo kwanza ili tupishe shamrashamra za michezo ya timu za taifa.

Kwenye wiki ya timu za taifa tutatarajia kumuona Mane yule wa EPL wakati akiwa na timu yake ya taifa wakicheza dhidi ya Congo Brazaville na kisha kwenda ugenini kuwakabili Eswatini kwenye michezo ya kundi I.

Nyota huyo yupo ndani ya timu ya taifa ya Senegal na safari hii atakuwa na vibarua viwili vya kuiwakilisha timu yake dhidi ya 

Wilfred Ndidi (Leicester City/Nigeria)

Kama kuna watu wanahitaji kupewa sifa kutokana na kiwango bora kabisa cha Leicester City msimu huu basi mmoja wao ni Wilfred Ndidi. Anapora na kusambaza mipira kwa ustadi wa hali ya juu kitu kinachowarahisishia kazi kina James Maddison na Youri Tilesman.

Wiki hii makali ya Ndidi yatahamia kwenye bara la Afrika ambapo yeye pamoja na Wanigeria wenzake watakuwa kwenye viwanja viwili tofauti kusaka alama dhidi ya Benin nyumbani na kisha Sierra Leone ugenini kwenye michezo ya kundi L.

Piere Aubamiyang (Arsenal/Gabon)

Nahodha mpya ndani ya kikosi cha Arsenal. Umuhimu wake ndani ya kikosi cha Washika Bunduki hauwezi kuelezeka. Msimu uliopita tu alikuwa mfungaji bora wa ligi licha ya kuwa timu yake haikufanya vizuri.

Hata hivi sasa tayari ameshafunga mabao 8 kwenye msimu huu na bado anaendeleza moto wake dhidi ya nyavu za timu pinzani.

Kwenye upande wa timu yake ya taifa mambo si mazuri sana hasa baada ya kukosa nafasi ya kushiriki Afcon iliyopita. Wiki hii wanainza safari nyingine ya kujaribu kushiriki kwa mara nyingine.

Aubamiyang atakuwa na nia ya kuleta kiwango chake kizuri kwa timu yake ya taifa wakati watakapokuwa wakikabiliana na DR Congo ugenini na kisha kuwakaribisha Angola kwenye michezo ya kundi D.

Wilfred Zaha (Crystal Palace/Ivory Coast)

Nyota wa timu ya Crystal Palace ambaye alikuwa na nafasi ya kuchezea timu ya taifa ya Uingereza hata hivyo akaamua kuchagua kucheza kwenye taifa lenye asili ya baba yake.

Amekuwa ni nguzo muhimu ndani ya kikosi cha Palace kwa misimu kadhaa sasa ndiyo maana sio ajabu kuona akihusishwa na usajili wa kutakiwa kujiunga na timu kubwa barani ulaya kwa pesa ndefu.

Wiki hii atakuwa kwenye jezi za Ivory Coast akiiwakilisha timu yake kwenye michezo ya kundi K ambapo kwanza watakuwa nyumbani dhidi ya Niger na kisha watakwenda ugenini dhidi ya Ethiopia.

Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria)

Winga huyo anayetumia zaidi mguu wake wa kulia msimu huu amekuwa hana nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha kocha Pep Guardiola. Hata hivyo bado ni mchezaji wakutegemewa zaidi kwenye taifa lake na amekuwa akifanya vizuri kila anapovaa jezi.

Kwenye Afcon iliyopita ambayo ilifanyika nchini Misri alikuwa ni sehemu ya kikosi ambacho kilifanikiwa kunyakuwa taji na kuweka rekodi yao ya kwanza kabisa kushinda ubingwa huo.

Wiki hii timu yake itakuwa na mechi mbili za kundi H ambazo ni dhidi ya Zambia nyumbani na kisha watasafiri kwenda kucheza dhidi ya Botswana.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya