Connect with us

Habari

Ziara: Wachezaji Na Viongozi Wa Singida United Walipotembelea Ofisi Za SportPesa

Spread the love

DAR ES SALAAM, Tanzania- Wachezaji wa Singida United siku ya jana ya Oktoba 16 walipata fursa ya kutembelea ofisi za kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ambao ni wadhamini wao wakuu kwa ajili ya kuweza kufahamiana na kubadilishana mawazo.

Wachezaji wa Singida united wakiongozwa na kocha mkuu Hans Van der Pluijm walifika kwenye ofisi za SportPesa majira ya saa tisa kamili alasiri ambapo walipokelewa na Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Bwana Tarimba Abbas.

Wachezaji wa SIngida United wakifuatilia somo kwa ukaribu zaidi

Moja ya shughuli ambazo ziliweza kufanyika wakati wa uwepo wao kwenye ofisi hizo ni pamoja na somo kwa wachezaji na viongozi kutoka kwa Meneja Mkuu wa Masoko, Kelvin Twissa lililojikita katika matumizi ya mitandao ya kijamii sambamba na kwa wachezaji kujiongezea thamani na kutengeneza nembo zao kibiashara kupitia majina yao.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Bwana tarimba Abbas (kushoto) akipokea jezi ya Singida United iliyosainiwa na wachezaji wa timu hiyo, Kulia ni Kocha Mkuu wa Singida United, Hans Van der Pluijm na katikati ni nahodha wa kikosi hicho, Nizar Khalfan. Picha /SPN

Sambamba na somo hilo, wachezaji wa Singida United walisaini jezi ambayo ilikabidhiwa kwa uongozi wa SportPesa ambapo Bwana Tarimba Abbas, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji akipokea kwa niaba.

Baada ya hapo lilifuata zoezi la upigaji dana dana kati ya wachezaji wa Singida United sambamba na wafanyakazi wa SportPesa na mwisho kabisa wageni na wenyeji wao wakajumuika kwa ajili ya picha ya pamoja.

Picha ya pamoja kati ya wachezaji na viongozi wa Singida United sambamba na viongozi wa SportPesa.

Singida United itakuwa ni timu ya pili kutembelea ofisi za SportPesa baada ya Simba SC kufanya hivyo Alhamisi ya wiki iliyopita ya Oktoba 12 kwa lengo hilo hilo la kufahamiana sambamba na kubadilishana mawazo.


Spread the love

More in Habari