Connect with us

Habari

Volleyball: Yaliyojiri Uwanja Wa Taifa, APR Ya Rwanda Ikitwaa Ubingwa Wa Nyerere Cup

Spread the love

APR ya Rwanda imefanikiwa kuibuka mabingwa wapya wa Nyerere Cup katika mchezo wa mpira wa wavu maarufu kama Volleyball baada ya kuigaragaza Jeshi Stars ya Tanzania kwa seti 3-0 kwenye mchezo wa fainali.

Katika fainali hiyo iliyopigwa siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa ndani wa Taifa, APR ambayo anachezea nyota mtanzania, Jackson Mmary, ilitawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kufanikiwa kuizima Jeshi Stars ambayo imekuwa ikifahamika kwa ubora wake kuzuia mashambulizi ya adui tangu kuanza kwa michuano hiyo.

Mshambuliaji wa Jeshi Stars (Jezi ya Machungwa-Juu), Abel Masunga akipeleka shambulizi kwenye upande wa APR katika mchezo wa fainali ambapo Jeshi Stars walilala kwa seti 3-0. Picha/Sport Eye

Mashindano hayo yalichukua siku tano, kwa kuzishirikisha timu wenyeji kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na wageni Rwanda , ambapo jumla ya timu 13 kwa wanaume zilichuana huku kwa upande wa wanawake zikiwa timu sita..

Timu za Wanaume zilikuwa katika makundi matatu ambapo Kundi A zilikuwepo timu za APR (Rwanda),Nyuki (Zanzibar), Chui, Mjimwema na Makongo zote kutoka Dar. Kundi B lilikuwa na Timu ya Jeshi Stars, JKT (Dar es salaam), Police (Zanzibar) na Kigoma na Kundi C Magereza Tanzania (Dar es salaam), Shinyanga (Shinyanga), Pentagon na Flowers (Arusha).

Mashabiki waliofika uwanja wa ndani wa taifa kushuhudia fainali ya Nyerere Cup kati ya APR na Jeshi Stars wanawake na wanaume siku ya Jumamosi. Picha/Sport Eye

Kwa upande wa wanawake wao walicheza kwa mfumo wa ligi kulikuwa na Jeshi Stars, Magereza Tanzania, JKT, Makongo, Mjimwema (Dar es salaam) na APR (Rwanda) .


Spread the love

More in Habari