Connect with us

Habari

Vita Baridi: “Fanya Yako Acha Kuizungumzia Chelsea, ” Conte Amjia Juu Mourinho

Spread the love

MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amesema kuwa bosi wa Manchester United, Jose Mourinho anatakiwa kujiangalia mwenyewe na sio kuizungumzia Chelsea.

Chelsea inakumbwa na majeruhi ambapo baada ya mchezo wa jana wa ligi ya mabingwa dhidi ya Roma ulioisha kwa sare ya 3-3 kwenye dimba la Stamford Bridge, Conte alisema kuwa timu yake hiyo inakumbwa na hali ya dharura.

Mourinho ambaye ameshaifundisha Chelsea kwa vipindi viwili tofauti amesema kuna makocha wanalia lia kutokana na wachezaji wao kuwa majeruhi.

“Mara nyingi Mourinho amekuwa akitazama na kuongelea mambo yanayotokea Chelsea,” Conte alisema.

Akiulizwa kuhusu kauli hiyo ya Mourinho ambayo haikuelekezwa kwake moja kwa moja, Kocha huyo wa zamani wa Juventus na timu ya taifa ya Italia alisema: “Ni mara nyingi, hata msimu uliopita, Nafikiri anatakiwa afikirie kuhusu timu yake na aache anachokifanya, ajiangalie mwenyewe na sio wenzake.”

David Luiz na Tiemoue Bakayoko walipata majeruhi kwenye mechi ya jana ambayo iliisha kwa sare ya mabao 3-3 huku United ikishinda 1-0 dhidi ya Benfica ugenini.

Wakati N’Golo Kante na Danny Drinkwater wakiwa majeruhi, Cesc Fabregas ndio kiungo pekee wa kati aliyebaki kwenye kikosi cha Chelsea kwa sasa.

“Wachezaji wale wale wamekuwa wakicheza tangu msimu wa maandalizi,” Conte alisema. “Sio kuhusu majeruhi bali ni kujaribu kucheza vizuri.

“Wachezaji watatu wana majeruhi, sio saba wala nane, lakini bado ni hali ya dharura kwetu,” alisema Conte


Spread the love

More in Habari