Connect with us

Habari

Tuna Siku Kumi za Kujipanga Na Kurekebisha Makosa Madogo Madogo -Emmanuel Okwi

Spread the love

DAR ES SALAAM, Tanzania – Mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Emmanuel Okwi amesema kikosi cha wekundu hao wa msimbazi bado kina nafasi ya kurekebisha makosa madogo madogo ili kuweza kuwa fiti kuelekea kwenye mchezo wa ngao ya jamii Agosti 23 dhidi ya Yanga.

Okwi ameyasema hayo wakati akiongea na SportPesa News baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya timu yake ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa jioni ya leo kwenye dimba la Taifa ambapo aliweza kufunga bao pekee na kuiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

“Kwa sasa hivi naona bado kuna makosa tunayafanya kama timu lakini bado tuna nafasi kama siku kumi hivi kujipanga vizuri na kurekebisha makosa madogo madogo lakini naona tukisharekebisha hayo makosa madogo tutakuwa timu nzuri”, alisema Okwi baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Fadhila

Hata hivyo Okwi hakuwa mchoyo wa fadhila baada ya kukishukuru kikosi kizima cha Simba kwa kumpa ushirikiano na hatimaye kuweza kuibuka na kufunga bao pekee kwenye mchezo huo wa leo.

“Kwanza ningependa kuwashukuru wachezaji wenzangu kwakuwa leo tumefanikiwa tena kupata ushindi kwani nisingeweza kufunga goli hili bila wachezaji wenzangu kwahiyo nashukuru kwa kunisaidia na kunipa pasi ya kufunga na najisikia vizuri sana”, alisema Okwi.

//platform.twitter.com/widgets.js

Yanga

Na je, vipi kuhusu mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga? Haya haya maneno ya Emmanuel Okwi.

“Simba kila tukiingia kwenye mechi tunahitaji ushindi na sisi tutaingia kwenye hiyo gmechi kupata ushindi”, alimalizia Okwi huku akiongea kwa kujiamini.

Bao pekee la Simba kwenye mchezo wa leo lilipatikana mnamo dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Emmanuel Okwi baada ya kumalizia vyema kazi nzuri iliyofanya na mshambuliaji mwenzake, John Bocco.


Spread the love

More in Habari