Connect with us

Habari

Tetesi: United Ipo Tayari Kumtoa Anthony Martial Ili Kumpata Ivan Rakitic

JINA la Anthony Martial limetanda kwenye vichwa vya habari za usajili kwa wiki kadhaa sasa.

Nyota huyo wa ufaransa ameshindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United kutokana na uwepo wa Marcus Rashford pamoja na Romelu Lukaku.

Kutokana na hali hiyo inayomkumba nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, inaelezwa kuwa Manchester United wapo kwenye mpango wa kutuma ofa kwa klabu ya Barcelona ambayo itamfanya Martial kwenda Barcelona na Ivan Rakitic kuja Manchester United. Gazeti la Star linaripoti.

Mourinho anaonekana kuwa tayari kupokea mchezaji mpya kama sehemu ya dili la kumuuza Martial ambapo Rakitic raia wa Croatia ndio chaguo namba moja kwake.

More in Habari