Connect with us

Habari

Simba Yawahimiza Wanachama Wake Kujitokeza Kwenye Mkutano Mkuu Kesho

Spread the love

DAR ES SALAAM, Tanzania -Klabu ya Simba inawatangazia Wanachama wake na wadau wa mchezo wa kandanda kote nchini kuwa Mkutano wake mkuu wa kawaida wa kila mwaka upo pale pale.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara, imethibitisha kuwa mkutano huo utafanyika kutokana na mahakama kufuta zuio la kuzuia mkutano huo

Hatua hiyo inafuatia na hukumu iliyosomwa jana katika Mahakama ya kisutu, kufuatia zuio la kuzuia Mkutano huo, liliowekwa na mmoja wa wadhamini wa klabu Mzee Hamis Kilomoni ambapo kwenye hukumu hiyo,mahakama ilitupilia mbali shauri hilo.

Mkutano huo utafanyika siku ya Jumapili tarehe 13-8-2017 (kesho) kuanzia saa nne kamili asubuhi, ukitanguliwa kwa wanachama wa klabu kujiandikisha kuanzia saa mbili kamili asubuhi.

Mabingwa hao wa kombe la FA, wameamua kufanyia mkutano huo kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere international Conference Centre) ambao upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha(IFM).

Uongozi wa Simba unawaomba wanachama wake kuhudhuria kwa wingi kwenye mkutano huo muhimu, huku mahitaji yote muhimu yakipatikana siku hiyo ikiwemo Vinywaji baridi na Chakula cha mchana.

Mwisho kabisa taarifa hiyo iliwataka wanachama wa klabu hiyo kwenda kutoa hoja kwenye mkutano huo.

Klabu inawaomba tena Wanachama wake wenye hoja tofauti waje kuzitoa ndani ya Mkutano huo kama inavyoagiza katiba ya klabu ikiwa ni mustakabali mzima wa maendeleo ya mchezo huu murua zaid nchini na kote Ulimwenguni”, ilieleza taarifa hiyo.


Spread the love

More in Habari