Connect with us

Habari

Samatta Atupia Mbili Genk Ikiibuka Na Ushindi Wa Mabao 5-3 Kunako Jupiler Pro League

Spread the love

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta leo ameibuka shujaa baada ya kuiongoza klabu yake ya Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi timu ya Royal Antwerp.

Wakiwa ugenini kwenye dimba la Bosuilstadion, Genk waliibuka na ushindi wa kwanza kwenye msimu huu mpya ambapo Mbwana Samatta alitupia magoli mawili.

Genk waliweza kuweka kimiani mabao manne ndani ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Samatta dakika ya 8 na 41, Leandro Trossard dakika ya 16 na Siebe Schrijvers dakika ya 21 huku Joarie Dequevy akifunga bao kwa upande wa Royal na mpira kwenda mapumziko matokeo yakiwa 4-1

Genk walipata bao ta tano kipindi cha pili baada ya Dino Arslanagic wa Royal kujifunga na kisha Royal wakaweza kupata mabao yao mengine mawili kupitia kwa William Owusu na Dino Arslanagic

Kwa matokeo hayo Genk wanapanda hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi hiyo maarufu kama Jupiler Pro huku ukiwa ni ushindi wao wa kwanza baada ya kutoa sare ya 3-3 dhidi ya Waasland Beveren kwenye mchezo wa ufunguzi huku pia wakipoteza mchezo uliofuata dhidi ya Standard Liege kwa mabao 2-1

Mchezo unaofuata Genk watakipiga na Charleroi nyumbani kwao kwenye dimba la Luminus Arena Agosti 19.


Spread the love

More in Habari