Connect with us

Habari

Ruvu Shooting Yaitungua Yanga Bao 1-0 Kwenye Mechi ya Kirafiki

Spread the love

DAR ES SALAAM, Tanzania -Klabu ya Yanga imepokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Ruvu Shooting kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la Chamazi jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa kujipima nguvu, bao pekee la Ruvu Shooting lilipatikana kipindi cha kwanza baada ya mlinzi mpya wa Yanga Abdullah Shaibu kujifunga kwa kichwa cha kuchumpa katika harakati za kuokoa krosi iliyopigwa na mchezaji wa Ruvu Shooting langoni mwake na hadi dakika 90 zinamalizika matokeo yalikuwa ni 1-0 kwa upande wa Ruvu Shooting.

Yanga wataondoka kesho asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar ambapo watacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Mlandege FC kwenye uwanja wa Amaan kabla ya kueleka Pemba kuweka kambi kujiandaa na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Simba.


Spread the love

More in Habari