Connect with us

Habari

Roman Abramovich Awaalika Matajiri Wa Kichina Kuwekeza Chelsea

Spread the love

LONDON, Uingereza- Klabu ya Chelsea imeanza mazungumzo na kampuni ya kichina juu ya uwekezaji wa paundi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika Stamford Bridge wiki iliyopita kama tovuti ya The Sun ya nchini Uingereza inavyoripoti, yaliwahusisha matajiri hao kutoka mashariki ya mbali pamoja na mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich.

Abramovich hana mpango wa kuuza hisa lakini inaelezwa kuwa anataka kuwa na wawekezaji ili kuiwezesha klabu kutotegemea pesa za mmiliki pekee.

Inaelezwa kuwa wafanyabiashara hao kutoka mashariki ya mbali wapo tayari kuweka mezani mzigo wa paundi milioni 500 ili kuwa sehemu ya ujenzi wa uwanja mpya, ambapo watalipwa pesa zao siku za usoni

Mchoro wa uwanja mpya wa Chelsea kama unavyoonekana kwa juu

Abramovich tayari ameshatumia kiasi cha paundi bilioni moja tangu alipoinunua Chelsea mwaka 2003 huku mabingwa hao wa Uingereza wakiwa hawana madeni.

Uwanja mpya wa Chelsea unatarajia kugharimu paundi milioni 500 na utajengwa eneo lile lile ambalo uwanja wa sasa wa Stamford Bridge ulipo.

Uwanja huo unatarajia kuchukua mashabiki 60,000 waliokaa huku ukiwa na matarajio ya kumalizika msimu wa 2021-22


Spread the love

More in Habari