Connect with us

Habari

Ngoma Hailali: Mrithi Wa Malinzi TFF Kuapishwa Leo Leo Baada Ya Uchaguzi

Spread the love

DODOMA, Tanzania -Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni, na Michezo, Mh. Dr. Harrison Mwakyembe amesema kuwa. Rais mpya wa TFF atakayechaguliwa leo, ataapishwa papo hapo tofauti na ilivyozoeleka miaka ya nyuma kuwa Rais huyo huapishwa siku chache baada ya kushinda uchaguzi.

Uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa Shirikisho la Soka nchini TFF akiwemo Rais, Makamu wa Rais pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji unatarajiwa kufanyika leo huko mjini Dodoma kwenye ukumbi wa St. Gasper ikiwa ni baada ya wagombea kuzinadi sera zao mbele ya wapiga kura kwa siku kadhaa sasa.

Uchaguzi huo unasimamiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli unafanyika baada ya Jamal Malinzi kuelekea kumaliza kipindi chake cha uongozi cha miaka minne.

Ukumbi wa St. Gasper ambapo ndipo uchaguzi mkuu wa TFF utakapofanyika kama unavyoonekana kwenye picha. Picha /TFF

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu na waandishi wa habari ambapo amesema Rais na wajumbe watakaopatikana leo wataapishwa mbele ya wapiga kura wote wa uchaguzi tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakisahau haki ya waliowachagua kwa kuwaapisha nje ya utaratibu.

Hata hivyo Waziri Mwakyembe aliwahimiza wajumbe kuwa makini katika suala zima la kuchagua viongozi leo huku akiwakumbusha sifa za kiongozi bora.

“Viongozi bora huchaguliwa na wajumbe makini wasioshawishika wala kuyumbishwa na tunataka viongozi ambao hawakumbatii rushwa kama ambavyo serikali, CAF na FIFA zinapingana na vitendo hivyo”, alisisitiza Waziri Mwakyembe.


Spread the love

More in Habari